Friday, July 04, 2014

BALOZI WA COMORO NCHINI ATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI



BALOZI WA COMORO NCHINI ATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI
Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Tanzania Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed Fakih ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kujitambulisha, kuangalia fursa na wigo wa kuanzisha mahusiano mazuri kati ya nchi yake na Hospitali hii. 

 Dkt. Mohammed amesema kuna Wacomoro wengi ambao wanapata huduma za tiba Hospitalini hapa hivyo ameona kuna haja na umuhimu wa pekee kuwa na uhusiano wa kiutendaji rasmi ili Watalaam kutoka Komoro waje kujifunza na kupata uzoefu wa utoaji huduma za tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Tanzania Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed Fakih akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bi. Agnes Mtawa.
Mh. Balozi akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mh. Balozi akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili mara tu baada ya ziara yake.