Wednesday, July 02, 2014

AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA II (AGRICULTURAL FIELD OFFICERS) – NAFASI 131




AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA II (AGRICULTURAL FIELD OFFICERS) – NAFASI 131
4.0 Afisa Kilimo Msaidizi Daraja La Ii (Agricultural Field Officers) – NAFASI 131
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
4.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kushirikiana na watafiti kuendesha vishamba vya majaribio,
• Kukusanya/kuhifadhi takwimu za majaribio,
• Kuwafundisha wakulima mbinu za kilimo bora,
• Kuwafikishia wakulima matokeo ya utafiti,
• Kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo, matumizi ya mbolea na madawa,
pembejeo za kilimo,
• Kukusanya na kutunza takwimu za mazao na bei kwa wiki mwezi, robo na
mwaka ngazi ya halmashauri,
• Kukusanya takwimu za mvua,
• Kushiriki katika savei za kilimo,
• Kushirikiana na vikundi vya wakulima kuhusu matatizo na teknolojia sahihi za
kutumia,
• Kupanga mipango ya uzalishaji,
• Kupima uotaji wa mbegu na kusimamia taratibu za ukaguzi,
• Kuwatambua wasambazaji wa pembejeo,
• Kutoa mafunzo ya lishe kwa wakulima,
• Kufanya vipimo vya ubora, unyevunyevu na uotaji wa mbegu,
• Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea,
• Kusimamia shughuli za kila siku za majaribio ya kilimo,
• Kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi bora ya udongo na maji,
• Kutoa ushauri wa kilimo mseto,
• Kuandaa sheria ndogo za hifadhi ya mazingira na
• Kutoa taaluma ya uzalishaji wa mboga, matunda, maua na viungo
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Sita (VI) wenye stashahada (Diploma) ya kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
4.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B Kwa mwezi.

Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 877 za kazi kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
-Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates. -Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI -Computer Certificate -Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards) -Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 11 Julai, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
 


APPLICATION INSTRUCTIONS:

Katibu
Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma
S. L. P 63100,
DAR ES SALAAM.