Sunday, June 29, 2014

VIJANA WALIOFADHILIWA MASOMO YA UFUNDI VETA NA HELP FOR UNDERSERVED COMMUNITIES INC. (HUC) WAHITIMU


VIJANA WALIOFADHILIWA MASOMO YA UFUNDI VETA NA HELP FOR UNDERSERVED COMMUNITIES INC. (HUC) WAHITIMU
 NI FURAHA TELE. Mwalimu wa kozi fupi wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma (VETA) – Dar es Salaam, Bi. Bertha Ogwal, kushoto, akimkabidhi Bi. Jamila Mwenda, ripoti ya mahudhurio ya kozi ya awali ya usekretari/kompyuta, hivi karibuni. Jamila ni miongoni mwa vijana 11 toka mikoa mbalimbali nchini waliofadhiliwa masomo na shirika lisilo la kiserikali la Help for Underserved Communities Inc. (HUC), lenye makao yake Marekani, ambalo linayosaidia upatikanaji wa maji safi na salama ya visima, maktaba za kijamii na ufadhili wa masomo ya ufundi. (Picha zote na Nathan Mpangala wa HUC).
 Mkuu wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma (VETA) – Dar es Salaam, Bw. Samuel Ng'andu wa pili toka kushoto, akimkabidhi cheti ya mafunzo ya awali ya ufundi magari, Yasini Musa hivi karibuni. Yasin ni mmoja wa vijana waliopata ufadhili toka shirika lisilo la kiserikali la Help for Underserved Communities Inc. (HUC). Wengine katika picha ni Msajili wa kozi Bi. Violet Fumbo na Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Kozi fupi Bw. Rocky Mongi.
 Kijana Joseph Mboya (kulia) akilamba ganda lake la ufundi magari toka kwa Mkuu wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma (VETA) – Dar es Salaam, Bw. Samuel Ng'andu, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
 Mwalimu wa Umeme wa magari wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma (VETA) – Dar es Salaam, Bw. Saidi Mbwana, akimkabidhi cheti ya mafunzo ya awali ya umeme wa magari, Bi. Neema Bungara jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Neema ni mmoja wa vijana  11 waliopata  ufadhili wa masomo ya ufundi toka shirika lisilo la kiserikali la Help for Underserved Communities Inc. (HUC).
HAKIKA WAKIWEZESHWA WANAWEZA. Bi. Neema Bungara akionesha ganda lake lililosheheni 'A' tupu. Neema ni mmoja wa vijana 11 waliopata ufadhili wa masomo ya ufundi toka shirika lisilo la kiserikali la Help for Underserved Communities Inc. (HUC).