JESHI la Polisi Zanzibar, linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kutekeleza shambulizi la bomu katika maeneo ya Darajani na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine saba kujeruhiwa.
Akizungumza na gazaeti hili ofisini kwake Ziwani, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa jeshi la polisi, DCI, Yussuf Ilembo ,alisema watuhumiwa hao walikamatwa Juni 18 mwaka huu majira ya usiku katika maeneo mbali mbali ya mi wa Zanzibar.
Hata hivyo, alikataa kutaja majina ya watuhumiwa hao akisema bado upelelezi unaendelea.
Alisema watuhumiwa wamepelekwa makao mkuu ya polisi Dar es Salaam kwa mahojiano.
Alisema watuhumiwa wamepelekwa makao mkuu ya polisi Dar es Salaam kwa mahojiano.
Aliwataka wananchi kuacha kufuata vishwawishi na kurubuniwa na watu au makundi ya kihalifu kwa lengo la kuchafua amani na kuwatia hofu wananchi.
Tukio hilo la bomu lilitokea wika Juni 13 majira ya saa 2:30 za usiku katika maeneo ya Darajani ya mjini Unguja na kuwalenga wahubiri wa amani wa dini ya kiislamu waliokuwa nje ya msikiti.
Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Kassim Issa Muhammed (36) ,Hamad Nassor Kassim (46) , Khelef Abdalla Abdalla (21), Khalid Ahmed Haidar (16) , Ahmed Haidar Jabir (47) na Suleiman Ali Juma (21) huku marehemu akitambulika kwa jina la Mohammed Khatib Mkombalaguha (26) mwenyeji wa Tanga.