Friday, June 27, 2014

Ujumbe wa leo

Kubweteka na Kujisahau ni Kitu Kibaya sana. Unakuta mtu alikuwa hana kazi anatafuta kazi anawaambia watu wamsaidie kutafuta kazi wanamsaidia kweli Mungu sio Filikunjombe jamaa anapata kazi. Wakati anaomba kazi anakuwa na unyenyekevu Yesu cha mtoto, jamaa mpaka machozi yanamtoka unavyoongea nae. Anapoanza kazi anakuwa na bidii sana anapata na kacheo kidogooo basi ghafla anabadilika ghafla yaani yeye ndo anajiona kama Mkurugenzi wa Kampuni anajiona yeye ndo yeye sana anakuwa mkaidi ananyanyasa wenzake pengine hata wale aliowakuta anasahau ndugu zake anasahau watu waliomfikisha hapo. Kama ndo Mume wako ama Mke wako anabadilika sana unatamani bora usingemsaidia kupata hiyo kazi anasahau kabisa majukumu anapata hiyo kazi anasahau kabisa kuwa kazi ni dhamana kabla ya yeye kuwepo hapo alikuwepo mwingine usibweteke kwa cheo cha kupewa. Ukibweteka kuna siku unaweza shangaa umerudi mule mule. Unasahau cheo ni dhamana.
Unaweza kuta mkaka wakati anafukuzia mdada anakuwa committed sana yaani kama ni simu anapiga mpaka basi mdada anashangaa anamkatisha tamaa lakini mdada anatamani kumchomolea lakini mshikaji anapiga simu mpaka mdada anaomba poo mpaka wanaongea wanamalizia na ile sauti "mambo mengine"ukiona watu wanaongea hiyo sentensi jua tu story zimeisha. Unakuta mkaka anabidii za kutosha kupeleka outing nini ghafla sasa akamuoa huyo mdada unashangaa mkaka anabweteka mbaya hampeleki tena outing zawadi ya mwisho ilikuwa walivyokuwa honeymoon miaka 5 imepita hakuna outings hakuna zawadi kumbe yote ile ilikuwa Chambo tu unabweteka unaona umeshapata ukianza kusaidiwa na wanaume wenzio kumpeleka mkeo outings usianze kukemea mapepo hakuna mapepo kama ulitaka kuoa usiogope gharama. Hela haileti mapenzi ila hela inaimarisha mapenzi hata kama ni kidogo ni kitu kizuri sana kwa mwanamke.
Mdada kabla ya kuolewa alikuwa anajiweka sopu sopu mbaya mpaka mkaka akadata unakuta baada ya kuolewa unabweteka, zamani kila ulipokuwa unakutana na mkaka unajipulizia pafyumu unaulambia unavaa nguo kaliiiii sasa ajabu ukiolewa unashindia mikanga kanga unashindia ma tshirt ya shingo panaaa utadhani unanyonyesha ule mvuto wa awali unapotea kabisa basi jua kabisa unakaribisha michepuko kwa mumeo. Unajua anakutana na akina nani huko ofisini?basi wewe Bweteka tuu.
Unakuta mtu kabla ya kupata kwenye maisha alikuwa mtu wa Mungu sana alikuwa anaomba kanisani hakosi ghafla sasa ameanza kupata amebadilika ameanza kuwa busy mbaya Kanisani tena imekuwa kama kwa mama Mkwe ambaye wanaugomvi. Unasahau kabla ya kupata hicho alichonacho alikuwa anashinda kwenye maombi anaomba utadhani mtoto wa Papa Paulo kumbe umasikini tu ulikuwa unamfanya mcha Mungu. Wengi wanampenda Mungu wakiwa na Frustrations za maisha wakishapata tu mananiii yanalia mbwaaataaaaa. Usibweteke kwa kile kidogo Mungu alichoanza kukupa kuna mengine mengi yako mbele yako.
Good Morning Teacher......