Friday, June 27, 2014

Kuna Njia kama Tano za kubaini Mtu mwenye Jeraha ndani yake.

Kwenye maisha yao. Assume ulikuwa unafanya kazi kwenye Kampuni fulani labda Marafiki Huru Company, baada ya muda ukafukuzwa kazi, sasa ukitaka kujua una maumivu
yasiyokuwa na hisia ni once unapokuwa umesikia habari njema ama mbaya za ile kampuni ndani ya moyo wako unajisikiaje ukiona unafurahia kuangamia kwake na kukasirika mafanikio yake basi jua unajeraha na jeraha la nafsi unapaswa uliepusha ndani yako.
Kuna Njia kama Tano za kubaini Mtu mwenye Jeraha ndani yake.
1. Kutokutaka Kuona/Kusikia Kuhusu kitu kilichomletea Jeraha-
Kama umewahi kuwa na majeraha yanayotokana na mahusiano, basi utakuta haupendi kusikia chochote
kinachomuhusu mwenzi wako wa zamani. Kama ni Kanisa hupendi sana kusikia habari zao
unaamini wewe kuwa salama ni kujiepusha nao lakini once akitokea Yule mpenzi wako
ghafla mmekutana mlimani city, moyo wako unararuka na unajikuta unatafuta njia ya kupita
ujiepushe nae. Ama kama unaona muito wa simu na kuangalia simu yako na kugundua ni mtu alijekujeruhi kwa namna moja ama nyingine, ukishaona unaanza kujipanga na kukunja uso kabla hujapokea na kuna fundo linakushika shingoni basi jua "Hayajaisha" hata kama unajikausha kwa kiwango gani.
2. Kupenda kusikia habari mbaya za Mtu/Kundi ama Jumuiya iliyokuletea Majeraha-
Unajisikiaje ndani ya nafis yako pale unaposikia mtu aliyeujeruhi moyo wako amepata ajali?moyoni unasema kisasi ni cha Bwana??au unasema Malipo ni hapa hapa duniani??ukiona
moyo wako unajisikia kupona unapopata habari mbaya kutoka kwa jamaa aliyekujeruhi
basi jua una jeraha ndani. Assume ungekuwa bado mna uhusiano wowote then baya
lingetokea ungejisikiaje?
3. Kujihami/kuchukua tahadhari kutokana na jambo hilo-
Kama umewahi kutana na mdada ambaye amejeruhiwa nafsi yake kwenye mahusiano, ukianza kumfukuzia cha kwanza anachojiandaa ni kuto kuumia tena, ukimwambia kuhusu mahusiano anakuwa mkali, utaona ana kutumia sms kali sana SITAKI MAHUSIANO NA WAKAKA au utasikia "FOR NOW AM NOT INTERESTING WITH MEN" kwa sisi wataalam tunajua hii ni
defence ya kuogopa kuguswa kidonda. Sasa kuna kasheshe ya kudate mdada ama mkaka
aliyewahi umizwa, njia nyepesi kwanza tibia jeraha kabla hujapanda kwenye moyo wake, vunja madhabahu za awali kisha jenga mpya, uki-ignore I tell you itakula kwako.
4. Chuki na Hasira Juu ya Chochote chenye kumletea Kumbukumbu ya zamani- Utakuta mtu kama ana picha anachoma moto kama ni nguo anachoma kama ni mtaa ndo umemsababishia hilo tatizo anahama, kama ni Kanisa ama mchungaji hataki kumuona. Ukimtazama hivi anakuwa kama yuko normal lakini kama mkapita sehemu ambayo imemsababishia jeraha unaweza kukuta ANASONYA ukimuuliza utasikia walaaa am just Ok. Kama kuna watu wanamsifia Mchumba wako waliyekujeruhi ama mtu aliyekuzima hela zako Kuna FUNDO la hasira huja kukaa kwenye koo, yaani unatamani umchane chane huyo mtu kama yuko mbele yako, unajikuta hutaki kukasirika lakini ndo unalo. Umewahi Kukutana na Mtu ambaye aliwahi pata ajali sehemu fulani ikatokea kila akipita eneo hilo anasisimka mwili mzima mpaka nywele zinasimama
5. Kupenda Kujitenga-
Mtu yeyote mwenye Jeraha anataka kukaa peke yake akiamini yeye ndo yuko salama. Unaweza kuta mtu mlizoea kuwa nae kwenda outing, mlizoea kuwa pamoja kabla ya kupata jeraha la nafsi mwisho wa siku unakuta mtu anabadilika, anatamani kukaa peke yake. Popote anaposikia "mbaya" wake yupo salama yake yeye ni kuto kukaa na huyo mtu ama group la hao watu. Hujawahi kumuona mtu mlikuwa kwenye Kamati Fulani pengine kutokana na Maneno ya Watu ama Yanayoendelea huyu mtu ghafla anatangaza "Kupumzika" kuwa mwana kamati, mnatafuta sababu hamuoni mkimuuliza anasema am just ok napumzika kwanza, basi jua katika sehemu ya ndani ya huyu mtu imeguswa na heri na salama kwake ni Kukaa mbali na nyie. Mpaka Jereha likitulia atawatafuta tena