Saturday, June 14, 2014

PEACOCK HOTEL YAWASHUKURU WAANDISHI WA HABARI KWA USHIRIKIANO



PEACOCK HOTEL YAWASHUKURU WAANDISHI WA HABARI KWA USHIRIKIANO
1Mkuerugenzi wa Hoteli ya Peacock ya jjini Dar es salaam Bw. Joseph Mlangila Mfugale ambaye ni mwekezaji mzawa katika masuala ya utalii akizungumza wakati wa hafla iliyoandaliwa na uongozi wa hoteli hiyo kwa waandishi wa habari kwa ajili ya kuwashukuru kutokana na ushirikiano ambao umekuwepo kwa muda mrefu na wanahabari, Mzee Mfugale amesema alianza na mtaji wa shilingi 800 na hadi sasa amewekeza zaidi ya shilingi bilioni 40 katika masuala ya hoteli na shughuli mbalimbali za kiutalii, Ameongeza kwa uwashukuru wateja wa hoteli hiyo na kuwakaribisha sana ili waendelee kutumia huduma za hoteli hiyo. 
2Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii TTB Bw. Geofrey Meena ambaye alikuwa ni mmoja wa wageni waalikwa akizungumza na kuupongeza uongozi wa hoteli ya Peacock kwa kazi nzuri wanayofanya katika kada ya Utalii.3Bw Damas Mfugale mmoja wa viongozi wa hoteli hiyo akitoa shukurani zake kwa wanahabari.4Baadhi ya wafanyakazi wa hoteli hiyo wakimwimbia wimbo mwenzao Vemila Njau wa pili kutoka kulia kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambayo iliambatana na hafla hiyo.5Mfanyakazi wa Hoteli hiyo Issabela Asenga akimkabidhi zawadi Vemilla Njau ikiwa ni kumpongeza kwa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.6Vemilla Njau akipuliza mishumaa kuzima mishumaa iliyowekwa kwenye keki yake wakati akipongezwa na wafanyakazi wenzake kwa kusherehekea siku ya kuzaliwa, aliyeshika keki ni Aisha Mwinjuma.7Vimella Njau akimbusu mfanyakazi mwenzake Aisha Mwinjuma wakati alipokuwa akipokea keki yake ya kusherekea siku yake ya kuzaliwa.9Baadhi ya wafanyakazi wa hoteli ya Peacock wakipozi kwa picha.10Dada Davina Meneja Masoko wa hoteli ya Peacockwa  pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake wakati wa hafla hiyo na wanahabari.12Wadau kutoka TTB kutoka kulia ni Mr. Deo, Geofrey Meena na Philip Gwihava mtangazaji kutoka Clouds TV.13Baadhi ya wanahabari wakiwa katika hafla hiyo.14Burudani kutoka kwa kundi la Wanne Star 15Baadhi ya wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo.16Wanahabari wakikaribishwa kwa kinywaji baridi.17Wageni waalikwa wakijadiliana mambo mbalimbali katika hafla hiyo.18Burudani ya muziki wa asili kutoka kwa Wanne Star.