Saturday, June 14, 2014

MAMA SALMA AWASILI KIGOMA KUADHIMISHA UCHANGIAJI DAMU



MAMA SALMA AWASILI KIGOMA KUADHIMISHA UCHANGIAJI DAMU


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa binti Mosi Kimosa ,7, anayesoma darasa la pili katika shule ya msingi Msimba iliyoko Kigoma Vijijini na binti Trisa Luziga,6, anayesoma darasa la kwanza mara baada ya Mama Salma kutua katika uwanja wa ndege wa Kigoma kwa ajili ya kumpokea Mama Salma aliyeenda mkoani huko


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mheshimiwa Issa Machibya akimpokea rasmi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma tarehe 13.6.2014. Mama Salma yuko mkoani humo kuhudhuria maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu salama duniani inayoadhimishwa kitaifa mkoani Kigoma



Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma za utamaduni zilizokuwa zikichezwa na akinamama wa Kigoma wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma kushiriki maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu salama duniani inayoadhimishwa kitaifa mkoani humo