Tuesday, June 17, 2014

Blue Leaf Mabingwa Safari Pool mkoa wa Lindi



Blue Leaf Mabingwa Safari Pool mkoa wa Lindi
KLABU ya mchezo wa Pool ya Blue Leaf Mkoani Lindi imemefanikiwa kutwaa Ubingwa wa fainali za mashindano ya mchezo huo yajulikanayo kama "Safari National Pool Competition 2014" uliomalizikamwishoni mwa wiki Mkoani humo na kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 800,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Lindi kwenye fainali za zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Bwalo la Polisi Pool Klabu na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/= na nafasi ya tatu ni Fisi Pool Klabu ambao walijinyakulia fedha taslimu Shilingi 250,000/=

Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaumeHassan Salum alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/= na nafasi ya pili ilichukuliwa na Pius Abubakari ambaye alizawadiwa Shilingi 250,000/= 

Mchezaji mmoja mmoja Wanawake, Mwajuma Othman alifanikiwa kutwaa ubingwa huo na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi300,000/= pamoja na kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa upande wa wanawake.Nafasi ya pili ilichukuliwa na Mariam Hassan ambaye alizawadiwa fedha taslimu Shilingi 200,000/=.

Fainali za kitaifa za 2014 za "Safari National Pool Competion" zinatarajiwa kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni Tabora,Shinyanga,DodomaMbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,
Manyara,Arusha,Tanga,Pwani,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.
Bingwa wa mchezo wa Pool Afrika upande wa mcvhezaji mmoja mmoja Wanaume(Singles), Patrick Nyangusi (kushoto) na Salum Ally wakishindana kucheza(Lag) wakati wa fainali za mchezo huo upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume uliochezwa katika klabu ya Jambo Lee Kawe jijini Dara es Salam mwishoni mwa wiki.Partick Nyangusi alishinda mchezo huo.
Mchezaji wa Klabu Pool ya Jaba, Kinondoni Dar es Salaam, Mayaula Muhagama akicheza wakati wa fainali zamchezo huo za mashindano yajulikanayo kama 'Safari National Pool Competition 2014" ngazi ya Mkoa,yaliyofanyika katika Klabu ya Jambo Lee Kawe Dar es Salaam.Kulia ni Mwamuzi wa mchezo huo, Peter Majani.