Sunday, May 18, 2014

Mkutano wa mashauriano ya uwekezaji wa awamu ya kwanza ya Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) waja

 
 
 
 
RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuongoza mkutano wa mashauriano ya uwekezaji wa awamu ya kwanza ya Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) ambao utawakutanisha wawekezaji mbalimbali wa ndani na nje kwenye kituo cha mikutano Mlimani City, jijini Dar es Salaam tarehe 3 na 4 juni,mwaka huu.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka Dar es salaam (DARY),Bi. Asteria Mlambo, amewaambia waandishi mwishoni mwa wiki kuwa mkutano huo wa mashaurino utatoa nafasi kwa wawekezaji kuzijua fursa mbalimbali za uwekezaji zitakazopatika kwenye mradi huounaojengwa kwa mabilioni ya pesa.
"Washiriki wote kwenye mkutano wa majadiliano watapata fursa ya kutembelea eneo la mradi na watapata nafasi ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wake kuhusu mradi," Bi. Mlambo alisema na kuongeza kuwa mkutano huo ni muhimu sana.
Akifafanua zaidi, Mtendaji huyo Mkuu alisema mabenki na taasisi mbalimbali za kifedha, makampuni ya kutengeneza mabasi, makampuni ya mawasiliano, mifuko ya kijamii na mengineyo mengi yamealikwa kwenye mkutano huo.
"Mada mbalimbali kuhusu mradi zitatolewa ambapo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw.Jumanne Sagini atawasilisha mada kuhusu mradi wa DART," alisisitiza.
Bi. Mlambo alisema kabla ya mkutano huo wa mashauriano mwezi ujao, Wakala ameanda mkutano ambao utaowakutanisha wamiliki wote wa daladala jijini Dar es Salaam pamoja na Kampuni ya Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) na wadau wengine ilikuwafahamisha kuhusu mkutano na kushaurina ni jinsi gani wataweza kunufaika na mfumo.
"Tutawaelezea faida na fursa zitakazopatikana kwenye mfumo mpya wa usafirishaji jijini na jinsi wao naowatakavyoweza kuwa sehemu ya mradi," alisema mtendaji mkuu huyo, na kuongeza kuwa taarifa na ratiba za mkutano zinapatikana kwenye tovuti ya wakala www.dart.go.tz.
Mwezi uliopita, wakala wa DART ulikamilisha zoezi la kusajili mabasi ya daladala yanayopita katika barabara ya Morogoro au kukatiza katika njia hiyo.
Hatua hiyo ya kuandikisha mabasi hayo ilikuwa moja ya matayarisho ya kupisha mradi huo wa mabasi yaendayo haraka.
Kwa sasa wakala huo uko kwenye mchakato wa kuwezesha upatikanaji wa watoa huduma kwenye mfumo mpya wa mabasi yaendayo haraka awamu ya kwanza ambayo inajumuisha barabara ya Morogoro, Kawawa na mtaa wa Msimbazi kwa njia kuu na nyingine za kiungo. Kulingana na mpango wa uendeshaji wa mfumo wa DART, barabara zinazohusika zitapaswa kutumiwa na mabasi ya mfumo huo pekee. Jumla ya njia 64 jijini Dar es Salaam zitakoma kutumika kutokana na kuanza kwa mradi huo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Bi. Asteria Mlambo akisisitiza akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, Jijini Dares Salaam juu ya muhimu wa mkutano wa mashauriano ya  uwekezaji wa awamu ya kwanza ya Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) ambao utawakutanisha wawekezaji mbalimbali wa ndani na nje kwenye kituo cha mikutano Mlimani City, jijini Dar es Salaam tarehe 3 na 4 juni,mwaka huu.Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais Jakaya Kikwete.