Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akiongoza Mkutano wa wananchama wa kundi la kwanza la Afrika katika mkutano wa IMF Jijini Tokyo-Japan
Waziri wa Fedha Mhe William Mgimwa akitoa maelekezo kwa Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma, Kamishina Msaidizi wa Fedha za Nje Bw. Jerome Bureta na Afisa mwandamizi Bw. Omary Khama Jijini Tokyo-Japan
Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu akisikiliza kwa makini mkutano wa IMF pamoja na maofisa waandamizi Bw. Omary Khama na Bw. Msafiri Nampesya Jijini Tokyo – Japan
Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akijadiliana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Harry Kitilya, Mkurugenzi Utafiti Uchumi na Sera Dk.Joseph Leina Masawe wa Benki Kuu ya Tanzania, Ofisa Mwandamizi Bw. Omary Khama na Bw. Cyprian kuyava wa Wizara ya Fedha baada ya mikutano hiyo ya IMF kwa siku ya leo hapa Jijini Tokyo- Japan.
Mhe. William Mgimwa akiwa na mtangazaji wa Shirika la NHK-SWAHILI Bi Anna Kwamba awali alikuwa (TBC) baada ya kumaliza mahojiano na Mhe. Waziri juu ya faida za mikutano ya IMF kwa wananchi wa Tanzania hapa Jijini Tokyo – Japan.
Mhe Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akiwa na Maafisa waandamizi wa wizara ya Fedha Bw. Omary Khama na Bw. Cyprian Kuyava Jijini Tokyo – Japan
Mhe Mgimwa akitoka kwenye mkutano na ujumbe alioambatana naye katika Mikutano ya IMF Jijini Tokyo- Japan
---
“Shirika la fedha la kimataifa (IMF) hujishughulisha na kutoa ushauri wa kisera kwa nchi wanachama na kutoa mikopo na misaada ya kifedha. Hayo yamesemwa na Mhe. Mgimwa jijini Tokyo- Japan. Akishiriki kikao cha kundi la Africa(African Group one Constituency),aidha, Mheshimiwa Mgimwa aliwasilisha hoja kwa niaba ya Magavana wa Afrika, na mbele ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IMF Bwana Shinowara, ya kulitaka shirika hilo kupunguza kiwango cha kigezo cha kukopa ili kuruhusu Nchi zinazoendelea kupata unafuu na kuziwezesha kukopa fedha za kufadhili kwa miundombinu ya Barabara, Reli na Bandari.
Mhe. Mgimwa alisema kuwa, mkutano huo uliangalia uhalisia na vigezo vinavyotolewa na Shirika la Fedha la kimataifa kuruhusu nchi wanachama kukopa tu katika ukomo wa sasa wa asilimia 35 na zaidi (Concesionality). Aliendelea kufafanua kwamba, jambo kubwa ni kuangalia jinsi ya kuboresha taratibu za kukopesha katika mikopo nafuu. Aidha, wajumbe wa mkutano wamekubaliana na haja ya kuwepo kwa utaratibu wa kuhakikisha kuwa nchi zote zinakuwa na madeni yanayohimilika”. Alisisitiza Mgimwa.
Wakijadiliana katika mkutano huo wajumbe hao wameshauri Shirika la fedha la kimataifa pamoja na taratibu zake, liangalie namna ya kulegeza masharti ya mikopo ili nchi wanachama ziweze kuboresha miundombinu.
“ IMF walau itizame aina ya miradi yenye chachu ya ukuwaji wa uchumi ambayo inaweza kutizamwa kwenye viwango vya ukopaji vya chini ya asilimia 35”.Aliongeza Mgimwa.
“Tunashukuru kuwa IMF imekuwa ikitupatia mikopo ya masharti nafuu, mikopo ile ya mapumziko ya miaka saba kabla ya kuanza kulipa na yenye riba ndogo sana na yenye masharti nafuu”. Mgimwa alisisitiza.
Akitolea mfano wa mradi wa gesi wa Tanzania, Mgimwa alisisitiza kuwa upatikanaji wa gesi utaongeza uzalishaji, ajira na viwanda. Kuongezeka kwa ajira kutaongeza kukua kwa pato la Taifa. Hii itasaidia kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa nchi ya Tanzania na hata Afrika kwa ujumla.
Mikutano hiyo bado inaendelea hapa jijini Tokyo-Japan na nchi wanachama wanaendelea kuja kwa wingi.
Imetolewa na Msemaji Mkuu -Wizara ya fedha
Bi. Ingiahedi Mduma
Tokyo-Japan
9oktoba 2012