Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh Freeman Mbowe akihutubia wananchi wa Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha jana.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh Freeman Mbowe akihutubia wananchi wa Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha jana katika muendelezo wa kampeni za chama chake kuwania nafasi ya uwakilishi katika Halmashauri ya Jiji kupitia Kata hiyo. Mkutano huo nusura usifanyike hiyo jana baada ya kilichoelezwa kuwa chama hicho kilikosa eneo la kufanyia mkutano na hivyo kulazimiaka kufanyia nje ya ofisi za chama hicho Kata ya Daraja Mbili, ofisi ambazo ziko jirani na za mahasimu wao kisiasa, CCM.Aidha, ujio wa Mbowe haukujulikana mapema kiasi cha wananchi kushangaa kumuona jukwaani ghafla tu. Pia, Mh Mbowe hakuweza kumnadi mgombea wa chama hicho kwa kuelezwa kwamba alikuwa anashikiliwa na Polisi alikolazwa hospitali ya Mt Meru na hivyo kushindwa kuhudhuria mkutano huo.
Godbless Lema nae akizungumza mkutanoni hapo.
Sehemu ya umati wa watu uliojitokeza kusikiliza hotuba za viongozi wa Chadema. Katika mkutano huo, zaidi ya sh laki 3 zilichangwa na wananchi hao kusaidia kampeni zaidi za chama hicho katika Kata hiyo.
PICHA / HABARI : KWA HISANI YA ARUSHA255 BLOG