Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Saada Mkuya Salim akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha.
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akizunguza machache na Wanachana na Wadau PPF wanaoshiriki kwenye Mkutano huo unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha leo hii.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh. Magesa Mulongo akitoa salamu zake na kuwakaribisha Wanachana na Wadau wote wa PPF waliofika kwenye Mkutano huo na kutaka kutokuwa na mashaka yeyote kwani kila kitu kinakwenda sawa kabisa chini ya uongozi wake.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PPF,Dk. Adolf Mkenda akitoa hotuba yake mapema leo asubuhi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau PPF unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF,William Eriyo akizungumza machache na kutoa utambulisho wa baadhi ya viongozi wakuu wa PPF wakati wa Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha leo.
Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Saada Mkuya Salim akikabidhi tuzo na Cheti cha ushindi kwa Meneja wa Fidia na Faida wa Benki ya CRDB,Anamen Shangali Mosha baada ya Benki hiyo kushika nafasi ya Pili kwenye Kipengele cha Sekta ya Fedha.
Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Saada Mkuya Salim akimabidhi tuzo kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania,Julius Angelo (pili kulia).Benki Kuu ndio walioibuka washindi wa Jumla wa tuzo hizo.
Wafanyakazi wa Benki Kuu wakiwa kwenye Picha cha Pamoja na Uongozi mzima ulopo meza kuu.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.