Watuhumiwa wa vurugu za Mbagala wiki iliyopita, wakiwa chini ya ulinzi wa polisi, walipofikishwa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza jana. Watuhumiwa 29, wawili kati yao wanawake, walisomewa mashtaka mbalimbali kuhusiana na vurugu zilizopelekea makanisa kadhaa kuchomwa moto wiki iliyopita, chanzo ikiwa ni baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa waislamu, kuandamana wakipinga mtoto mmoja kukojolea Quraan tukufu. Dhamana ya watu hao itaamuliwa Oktoba 30.
|
Baadhi ya watuhumiwa wa vurugu zilizotokea Mbagala jijini Dar es Salaam wiki iliyoipita, wakiwa ndani ya gari la polisi walipofikishwa mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Oktoba 16, 2012 kwa mara ya kwanza. Watuhumiwa 29, wawili kati yao wanawake, walisomewa mashtaka mbalimbali kuhusiana na vurugu zilizopelekea makanisa kadhaa kuchomwa moto wiki iliyopita, chanzo ikiwa ni baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa waislamu, kuandamana wakipinga mtoto mmoja kukojolea Quraan tukufu. Dhamana ya watu hao itaamuliwa Oktoba 30. |
|
Akina mama wanaotuhumiwa kuhusika na vurugu zilizotokea huko Mbagala, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita, wakishuka kutoka ndani ya gari la polisi kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana. Akina mama hao ni miongoni mwa watuhumiwa 29 waliofikishwa kwenye mahakama hiyo kujibu mashtaka ya kuhusika na vurugu za kuvamia makanisa, kuchoma, kuharibu mali na kuiba. |
|