Saturday, September 29, 2012

WAKRISTO WATAKIWA KUONGEZA MAOMBI BAADA YA USHINDI.


 Watu waliokata shauri katika semina hiyo wakiombewa maombi na Askofu Laurent Magike leo.
                                         Nguvu ya Mungu akifanya kazi.
                        Upako wa Mungu wa kung'oa kila pando la shetanii.
 Operesheni kufukuza shetani hapaaa ikiendelea kwa bidii zote, hapa utasikia maneno shetani toka, shetani umeshindwa na n.k.

                      Living Water kwaya wakiimba seminani hapo kanisani.

Wakristo wamekumbushwa kutinza ushindi, baraka walizozipata kwa Mungu baada ya kuokoka na kuombewa kwa Jina la Yesu Kristo na kuendelea kuongeza maombi zaidi.

Hayo yamesemwa na Askofu Laurent Magike wa Huduma ya Living Water International Ministries leo katika semina kubwa ya neno la Mungu katika Kanisa hilo lililopo Kiseke Jijini Mwanza.

Amesema wakristo wengi wamekuwa wakijisahau kuwa shetani na majeshi yake yuko kazini na nia yake kuu ni kutaka kumwangusha mkristo hasa ambaye alikuwa akitumikishwa na shetani.

Amesema kuwa wakristo wengi wamekuwa wakishindwa kuulinda ushindi walioupata kwa damu ya Yesu pale msalabani kwa sababu wamekuwa wakimpa shetani nafasi sana katika maisha yao baada ya kuokoka kutoka utumwani mwa shetani.

Pia amesema kuwa shetani mara zote amekuwa akipanga mbinu za kumharibu mkristo hasa baada ya kukemewa na kutoka kwa Jina la Yesu na shetani sikuzote amekuwa mstari wa mbele kutaka kumrudisha mkristo nyuma.

Ametoa ushauri kwa kila mkristo kusoma neno la Mungu kwa bidi na kuzidisha maombi maana ndiyo mguzo muhimu za mkristo yeyote aliye na mpango wa kwenda mbinguni.