Tuesday, September 25, 2012

UFUNGUZI WA WIKI YA WAHANDISI SEPTEMBA 24 – 28, 2012 MKOA WA DODOMA



Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akipata maelezo ya kitaalamu juu ya mabadiliko mbalimbali ya teknplojia ya vyombo vya kusafirisha mawasiliano tangu miaka ya zamani kutoka kwa Mtaalamu wa Mawasiliano wa kampuni ya simu TTCL Bw. Innocent Mbosa (mwenye kofia) wakati wa uzinduzi wa wiki ya wahandisi katika viwanja vya Nyerere Dodoma jana.
Mtaalamu wa Miundombinu na mifumo ya usambazaji maji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mjini Dodoma – DUWASA Bw. Revocatus Nsubile akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (mwenye kilemba) vifaa vinavyotumika katika usambazaji maji wakati wa sherehe za ufunguzi wa wiki ya wahandisi Kimkoa katika Viwanja vya Nyerere Mjini Dodoma jana.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akizungumza na Watendaji wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dodoma juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hususani Ujenzi wa barabara ya Dodoma Iringa na Dodoma Bonga Manyara wakati wa sherehe za ufunguzi wa wiki ya wahandisi Kimkoa katika Viwanja vya Nyerere Mjini Dodoma jana.  
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akizungumza na wahandisi wa fani mbalimbali,viongozi na wananchi wa Dodoma waliofika uwanja wa Mwl. Nyerere wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Wahandisi.
Baadhi ya wasanii wa kikundi cha ngoma na sarakasi cha Hiari ya Moyo cha Mjini Dodoma wakitumbuiza wakati wa sherehe za ufunguzi wa wiki ya wahandisi Kimkoa katika Viwanja vya Nyerere Mjini Dodoma jana
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Tawi la Dodoma Bi. Maria Sasabo (mwenye kofia) akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kushoto) Televisheni ya Digitali na ile ya Analojia ikiwa ni sehemu ya kutoa elimu juu ya mabadiliko ya Mfumo wa utangazaji toka Analojia kwenda Digitali wakati wa sherehe za ufunguzi wa wiki ya wahandisi Kimkoa katika Viwanja vya Nyerere Mjini Dodoma jana.
Mhandisi Mazingira wa Manispaa ya Dodoma Bw. Barnabas Faida (Kushoto) akitoa maelezo ya kitaalamu kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kulia) juu ya utafutaji wa maji kwa vyanzo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa wiki ya wahandisi katika viwanja vya Nyerere Dodoma jana.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wanachama wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET) Tawi la Dodoma muda mfupi baada ya kufungua wiki ya wahandisi kwenye viwanja vya Nyerere Mjini Dodoma.