Tuesday, September 11, 2012

Treni ya kwanza ya Dar-Ubungo yafanyiwa majaribio


 
 Kichwa cha treni pamoja na mabehewa sita ya awamu ya kwanza,yakisubiri kufanyiwa majaribio kwa  Safari zitazoanzia Station ya Dar es Salaam Mpaka Ubungo mnamo mwezi wa kumi. Majaribia hayo yameongozwa  na Naibu Waziri wa Uchukuzi,Mhe. Dk Charles Tizeba(Mb) ambaye alipanda treni hiyo kuanzia Station Dar es Salaam Mpaka Ubungo.Serikali imetumia kiasi cha Sh. Bil 4.75 kwa ajili ya ukarabati wa njia,injini na mabehewa.
 
 Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(Mb),akipanda treni wakati wa majaribio ya Mabehewa sita ya treni kati ya mabehewa kumi na mbili yanatogemewa kutumika na Shirika la reli Tanzania(TRL). Treni hizo  zitakayofanya safari zake kutoka Station Dar es Salaam mpaka Ubungo,mapema mwezi wa Kumi.
 
  Baadhi ya wananchi wakipanda katika behewa moja kati ya Sita yaliyofanyiwa majaribio mapema leo kutokea Station mpaka Ubungo(km 12).
 
 Mchuma huo unaondoka
 
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania(TRL) wakiwa na furaha ndani ya mojawapo ya mabehewa yaliyofanyiwa majaribio leo abubuhi.
 
 Abiria wa majaribio