Sunday, September 30, 2012

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Willbroad Slaa amepokea wanachama wapya kutoka familia ya mwanasiasa mkongwe nchini na Waziri wa Nchi 0fisi ya Rais(Mahusiano na Uratibu) Mh Stephen Wasira,Estha Wasira na Lilian Wasira.



Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, akiwakabidhi kadi ya uwanachama wa chama hicho kwa Lilian Wassira na ndugu yake Esther, baada kujiunga na chama hicho. Lilian na Esther ni watoto wa George Wassira Kaka wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano) Stephen Wassira.Picha na Michael Matemanga-Mwananchi)
-----
Baada ya kamanda Makongoro Wasira kujiunga na M4C siku chache zilizopita, leo tena watoto wengine wa Wasira wamejiunga na M4C na kukitupia virago Chama cha Baba yao CCM. Waliojiunga leo katika Makao makuu ya Chadema na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa ni kamanda Ester Wasira na Lilian Wasira.

Lilian Wasira (Mwanasheria, graduate wa TUDARCO):(i) Alielezea furaha yake kwa kujiunga na chama makini na chenye kuleta matumaini mapya kwa Mtanzania

(ii) Aliwaasa vijana, akina mama na wazee wajiandikishe kwa wingi nafasi itakapotokea na 2015 wakamalizie kazi ya ukombozi kwa kuipigia CHADEMA kura

(iii) Amewaasa Watanzania kuacha kulalamikia maovu ya CCM na kuchukua hatua ya kuiweka CCM pembeni na kuleta Chadema kama chama mbadala. Alisema hakuna sababu ya kuwa na mfumo wa vyama vingi kama watanzania hawathubutu kuchagua chama mbadala na badala yake kuendelea kuichagua CCM na kulalamika kila siku kuwa CCM imeshindwa kuongoza nchi.

(iv) Kwamba CCM imekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 hivyo ni wakati sasa wa kuiweka pembeni na kuingiza chama kipya, mawazo mapya na kujenga mfumo mpya wa uongozi. Hakuna kitu CCM imeshindwa kufanya kwa miaka 50 inaweza kufanya kwa miaka 5 au 10 ijayo.

(v) Anasema ana imani na sera za chadema kuwa ndizo zitatukomboa. Amewapa moyo viongozi wa CHADEMA wasitishwe na vitisho na mauaji yanayofanywa na dola na kusema yupo tayari kwa M4C na yupo tayari kulipuliwa kama walivyolipuliwa wanachadema wengine na kuuawa kama itambidi afanye hivyo.

(vi) Kwamba CHADEMA ni Chama kinachosubiri kuingia Ikulu isipokuwa tu watu wajiandikishe, wapige kura na walinde kura.

(vii) Naye alimalizia kwa kusema, “Kwa msaada wa Mungu Tanzania mpya inakuja.” Dkt. Slaa alitiwa moyo sana na ujasiri ulioonyeshwa na vijana hawa pamoja na maneno ya kizalendo waliyoongea na akawakarisha kwenye uwanja wa mapambano ya M4C.