Wednesday, September 12, 2012

Harambee Ya Mjane Wa Daud Mwangosi; Utaratibu Wa Kupokea Michango Ya Kijumuiya...


by 

 
Ndugu zangu,
Wengi wameendelea kuitikia wito wa kumchangia mjane wa marehemu  mwandishi Daud Mwangosi .

Imeanza pia kujitokeza michango ya kijumuiya. Ni jambo jema sana. Hata hivyo, ili  kuepuka kuchanganya siasa kwenye suala hili la kijamii  na la kibinadamu katika kumsaidia mjane wa marehemu, kama mratibu wa harambee hii, napendekeza kuanzia sasa wale wote watakaochangishana kijumuiya, hususan za  kiitikadi, basi, michango yao iwakilishwe hapa kama michango ya kutoka Jumuiya za Watanzania, popote pale walipo hapa duniani.

Natumia fursa hii pia, kwa kutambua kuwa kuna jumuiya mbali mbali za Watanzania, na za marafiki wa Tanzania  kwenye karibu kila kona ya dunia hii, kuwaomba wenyeviti wa jumuiya hizo kukusanya japo michango midogo kwa Wanajumuiya wenzao, iwe  Watanzania au marafiki wa Tanzania,  walio na utayari wa kuchangia hata kiasi kidogo tu cha pesa kwa mjane wa  marehemu. 

Michango hiyo inaweza kuwasilishwa kwangu kwa njia zifuatazo; M-Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money au NMB Mobile. Kwa namba 0754 678 252, 0712 95 61 31, 0788 111 765 ( Kwa walio nje mnaweza kutuma kwa Western Union, jina la mpokeaji- Maggid Mjengwa, Tafadhali nijulishe kama utatuma kwa njia ya Western Union )

Natanguliza shukran,

Maggid Mjengwa.