Mwenyekiti
wa Kijiji cha Emairete, Moran Poyoni, akimkabidhi zawadi ya fimbo
maalumu Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Samsung, Choi Woo-Soo, wakati wa
hafla ya kukabidhi madarasa kwa shule ya Irmorijo, yaliyokarabatiwa na
Kampuni ya Samsung na kutangaza msaada wa milioni 144 kwa shule hiyo na
Sekondari ya Winning Sprit Monduli Arusha jana.
Mama
wa Kimasai akimpa zawadi Dada wa Kikorea wakati wa hafla ya kukabidhi
madarasa kwa shule ya Irmorijo baada ya ukarabati uliofanywa na Kampuni
ya Samsung na kutangaza msaada wa Sh. milioni 144 kwa shule hiyo na
Sekondari ya Winning Sprit Monduli Arusha jana.
Makamu
wa Rais wa Samsung, Choi Woo-Soo (katikati), Mkuu wa Wilaya ya Monduli,
Joika Kasunga na Diwani wa Kata ya Monduli juu, Bariki Sumuni
wakishangilia baada ya kukata utepe kwa pamoja kuashira uzinduzi wa
madarasa ya Shule ya Msingi ya Irmorijo Monduli Arusha, yaliyokarabatiwa
na Kampuni ya Samsung na kuzinduliwa rasmi jana.
Wakinamama
wa Kimasai wa Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli, wakimkabidhi zawadi
ya Mbuzi, Makamu wa Rais wa Samsung, Choi Woo-Soo wakati wa hafla ya
kukabidhi madarasa kwa shule ya Irmorijo.
Makamu
wa Rais wa Samsung, Choi Woo-Soo akiwa katika vazi la Kimasai huku
akionyesha zawadi ya fimbo maalum aliyokabidhiwa wakati wa hafla ya
kukabidhi madarasa kwa shule ya Irmorij.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
KITENGO
cha biashara na ufumbuzi cha kampuni ya Samsung Electronics kimetangaza
mpango wa msaada wa shilingi za kitanzania milioni 144 sawa na dola za
Kimarekani 90,000 kwa ajili ya kusaidia shule ya msingi Ilmorijo na
shule ya sekondari ya Winning Spirit za Wilaya ya Monduli jijini Arusha.
Makamu
wa Rais wa Samsung Bw. Choi Woo-Soo alisema kuwa hii ni sehemu tu ya
mpango endelevu wa kusaidia jamii wa kampuni ya Samsung Electronics
kuwekeza katika elimu ndani ya nchi za Afrika.
“Sekta
ya elimu ni kipaumbele kikubwa kwetu kama Samsung na tutaendelea
kuwekeza katika sekta hii nchini Tanzania na bara la afrika kwa ujumla
kwa sababu bila ya elimu nchi haiwezi kupata maendeleo ya kiuchumi na
viongozi bora na sio bora viongozi,” alisisitiza makamu wa Rais wa
kampuni ya Samsung Wilaya ya Monduli, jijini arusha wiki hii.
Kampuni
ya Samsung ilikabidhi nyumba mbili za walimu zenye uwezo wa kukaa
familia nne za walimu na madarasa manne ya shule ya Msingi ya Ilmorijo.
Shule
hiyo itapata msaada wa kitaaluma na pia matengenezo ya majengo. Hii
inajumuisha baadhi ya wanafunzi kulipiwa gharama za shule, kuongezeka
kwa idadi ya walimu shuleni, kuongezeka kwa madarasa ya masomo ya ziada,
ushauri nasaha kwa familia na mipango mbalimbali ya elimu ya afya.
Bw
Woo-Soo alifafanua kuwa Samsung itakuwa ikifanya matengenezo na
kurekebisha huduma mbalimbali shuleni, fenicha na vifaa vingine pamoja
na kuwapatia wanafunzi chakula cha mchana kilichoboreshwa zaidi.
Kwa
mujibu wa afisa huyo, shule ya kuendeleza vipaji vya michezo ya watoto
ya Winning Spirit iliyoko jijini Arusha itapata nafasi ya kutoa
mwanafunzi mmoja ambaye atalipiwa gharama za masomo na kupewa mafunzo ya
riadha.
Mkakati
huu utasaidia kuunda watoto wenye vipaji ambao watapata usaidizi wa
kampuni ya Samsung na kuwa wanamichezo bora nchini na duniani.
“Tumejizatiti kuweka tofauti ya wazi kabisa katika maeneo ambayo wateja wetu wanaishi” alisema Bw. Woo-Soo.
Aliogeza
kuwa huu ni uthibitisho wa miradi waliyoianzisha katika maeneo mengi ya
bara la Afrika katika sekta ya elimu, kuunganisha vijiji na mahitaji ya
kimsingi ya jamii.
Mipango
ya kuitumikia jamii inayofanywa na kampuni ya Samsung katika bara la
Afrika inalenga kujenga miradi endelevu inayofikia mahitaji halisi ya
jamii husika kwa kuzingatia uchumi wao, asisitiza Bw. Woo-Soo.
Mradi
unaoaminika zaidi katika mpango huu ni Samsung Electronics Engineering
Academy, huu umetekelezwa kukidhi haja ya kuendeleza mafundi wenye ujuzi
ambao watakuwa watoa huduma bora waliowezeshwa ili kuzalisha mali na
kuinua uchumi.
Mradi
wa programu hii umeanzishwa katika nchi za Afrika ya Kusini, Kenya na
Nigeria kwa lengo la kutatua tatizo la upungufu wa wataalamu na mafundi
katika Afrika kwa kutoa mafunzo ya ufundi kwa vitendo kwa wanafunzi wa
shule za sekondari.
Katika
programu hii wanafunzi wanapatiwa mpango wa masomo ya ufundi kwa mwaka
mmoja, mafunzo haya hujumuishwa katika mitaala ya masomo ya ufundi.
Miradi
ya elimu ya kampuni ya Samsung pamoja na mipango ya wafanyakazi
kujitolea ni sehemu ya lengo kuu la kampuni hii inagusa moja kwa moja
maisha ya watu milioni tano katika bara la Afrika kufikia mwaka 2015.
“Tunaunganisha
uwezo wetu katika ubunifu ili kubadilisha jamii na maisha kuwa bora
zaidi, kutunza sayari yetu kwa ajili ya vizazi vijavyo na kufungua
nafasi za mafanikio kwa watu,” alinena kiongozi huyo wa Samsung.
Mipango
ya kuitumikia jamii ya kampuni ya Samsung katika bara la Afrika
inaendana na mpango wa global ‘Hope for Children’ initiative, ambao
unafanya dunia kuona haja ya kuboresha elimu na afya ya watoto katika
jitihada za kuboresha maisha ya watu na jamii.