Mwenyekiti
wa Tume ya Mabdiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Jospeh Warioba, akiongea
na Wawakilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri
waliofika ofisi za Tume jijini Dar es salaam jana (Jumanne, Agosti 14,
2012) kubadilishana mawazo. Kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Tume,
Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Katibu wa MCT, Bw. Kajubi
Mukajanga. Kulia ni Katibu wa Tume Bw. Rashid Assaaa.
Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba (katikati)
akimtambulisha Mwandishi wa Habari Mkongwe, Bw. Ahmed Rajab (wa pili
kushoto) kwa Wajumbe wa Tume. Kulia ni makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji
Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na kushoto ni Mjumbe wa Tume, Dkt.
salim Ahmed Salim (kushoto) na Katibu wa Tume, Bw. Rashid Assaa. Bw.
Rajab alikutana na Wajumbe wa Tume kubadilishana mawazo katika ofisi za
Tume jijini Dar es Salaam jana(Jumanne, Agosti 14, 2012).
Katibu
wa Jukwaa la Wahariri Bw. Neville Meena (kulia) akiongea katika mkutano
wa kubadilishana mawazo na uongozi wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam jana.
Waandishi
wa Habari Wakongwe, Bi. Pili Mtambalike (kulia), Bw. Allan Lawa
(katikati) na Bw. Suleiman Seif wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Jospeh Warioba, akiongea na
Wawakilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri
waliofika ofisi za Tume jijini Dar es salaam jana.
Baadhi
ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano kati ya Mwenyekiti wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Jospeh Warioba na Wawakilishi wa
Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri waliofika ofisi za
Tume jijini Dar es salaam jana.(Picha na Tume ya Katiba)