Tuesday, July 31, 2012

OLYMPICS London 2012


 
Bondia wa Tanzania Selamani Kidunda mwenye fulana nyekundu akiwa na viongozi na baadhi ya wadau wa michezo wakati akienda kupigana na Bondia toka Moldova  BELOUS Vasilii, Kidunda alipoteza mchezo huo kwa point 7-20.
 

Baadhi ya viongozi wa michezo walioko London, kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa michezo nchini Ndg.Thadeo, Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Ndg.Gullam, Makamu wa Rais wa Kikapu Tanzania Ndg.Magesa na Kiongozi wa msafara wa timu ya Tanzania Ndg. Jarufu.
 

Wadau wa michezo walioko London, kutoka kushoto Ndg. Amosi Msanjila afisa wa ubalozi London, Mtangazaji maarufu wa BBC Ndg. Charles Hilary, Makamu wa Rais wa TBF Ndg. Phares Magesa, na Mchambuzi mahiri wa Michezo wa BBC na mmliki wa tanzaniasports.com Ndg. Israel Sari