Wednesday, September 26, 2012

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA DAUDI MWANGOSI AFIKISHWA TENA MAHAKAMANI LEO


Mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daud Mwangosi  leo amefikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi ya Wilaya kujibu shitaka lilalomkabili.Huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari.
Akisomewa shitaka lake na  mwendesha mashtaka wa serikali Mkuu lilian ngilangwa , amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni askari mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) mkazi wa FFU Iringa, anakabiliwa na shitakala la mauaji ya makusudi.
Amesema mtuhumiwa huyo mnamo 02 Septemba mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.

Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya Dyness Lyimo mtuhumumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza kesi za mauaji.

Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana.
Mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na kesi hiyo imeahirishwa hadi 10 Oktoba  mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Hata hivyo askari wengi waliompeleka mtuhumiwa huyo wakiwa wamevaa nguo za kiraia walihakikisha kuwa mtuhumiwa huyo hapigwi picha jambalo limewaletea ugumu waandishi waliokuwapo baada ya kusukumwa ovyo kuzuia mtuhumiwa huyo asipigwe picha.

Kila wakati waandishi walipotaka kupika picha walikuwa wakisukumwa na askari hao huku mtuhumiwa akiwa amejifunika kichwa na kuvaa miwani meusi kuhakikisha kuwa sura yake haionekani na waandishi hao.

Katika hali isiyo ya kawaida mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo kwa gari binafsi la kifahari lenye namba za usajili DFP 2175 Toyota Land cruiser tofauti na watuhumiwa wengine ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa gari la polisi.