Wednesday, September 26, 2012

Breaking Nyuzzzzzzz: Watanzania Ugiriki wavamiwa na kupigwa


Sehemu ya uharibifu uliofanywa na wavamizi hao huko Ugiriki usiku wa kuamkia leo

Habari ankal Asante kwa kuniwekea habari zangu nyingi kuhusu Ugiriki, licha ya baadhi ya watu kuona tunawabania kuja Ugiriki na kuuliza kwa nini nyie mpo kama kuna matatizo Ukweli ni huu Chama cha XRISI AVGI au Golden down(Neo Nazi) kimeanza piga piga ya wageni wakiongozwa na wabunge wao ambao polisi inashindwa kuingilia kati wakiwepo.

Yaani usiku wa kuamkia leo   Septemba 26, 2012  ofisi za Jumuiya ya watanzania ziliharibiwa vibaya na baadhi ya watu kujeruhiwa. Licha ya kuwepo kwa Polisi bado walishindwa kuzuia tukio hilo na kuonekana polisi wakiwapa mgongo kabisa Watanzania baada ya hapo walielekea maeneo mengine ya mabaa ya wageni yaliyopo karibu na kuharibiwa vibaya pia Baadhi tu ya picha na news pia zipo kwenye mitandao mingi tu.

Mdau Umangani

Wadau wkiwa nje ya ofisi za Jumuiya iliyovamiwa