Wednesday, September 26, 2012

Rais Kikwete awaapisha Mnadhimu Mkuu wa JWTZ na Mkuu wa JWTZ leo Ikulu Dar es salaam



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha  Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba leo Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimjuapisha Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Shamsi Vuai Nahoda na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange  katika picha ya pamoja na Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja  Jenerali Raphael Mugoya Muhuga
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama na waapishwa
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika picha pamoja na Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba na familia yake baada ya kiapo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga na familia yake baada ya kiapo.

Luteni Jenerali Ndomba, aliyekuwa Mkuu wa JKT,  anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahman  A. Shimbo ambaye amestaafu Jeshi kwa mujibu wa sheria baada ya kufikisha umri wa miaka 60. 

Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga alikuwa Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).