Sunday, July 22, 2012

Meli ya Kisasa Kuzinduliwa Karibuni na Kampuni ya Azam Marine


KAMPUNI ya Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa ya kisasa kwa ajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja. 

Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka huu meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa. Mohamedi alisema shida ya usafiri itapungua kwa asilimia kubwa kutokana na meli hiyo kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1500, Mizigo tani 500 na magari 200 ambapo abiria atakae jisikia kwenda na gari lake Zanzibar, Pemba au Dar es Salaam ataweza kufanya hivyo. 

Waziri Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu na siyakutengeneza faida. Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20