Friday, July 15, 2016

WANANCHI SASA WANAWEZA KULIPA KODI ZA TRA POPOTE KWA KUTUMIA NMB.



WANANCHI SASA WANAWEZA KULIPA KODI ZA TRA POPOTE KWA KUTUMIA NMB.
Mkuu wa Kitengo cha Miamala Benki ya NMB, Michael Mungure (kulia) akipeana mkono na Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi TRA, Ramadhan Sengati mara baada ya kuingia makubaliano leo Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Kwa makubaliano hayo sasa mwananchi anaweza kulipa malipo ya kodi mbalimbali za Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kutumia mfumo wa Benki ya NMB 'NMB Mobile' au moja kwa moja kwenye tawi la NMB popote. Kushoto ni Meneja Huduma za Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili akishuhudia. Meneja Huduma za Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili akifafanua jambo wakati wa hafla ya kuingia makubaliano na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kukusanya kodi za TRA kupitia mfumo wa Benki ya NMB. Katikati ni Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi TRA, Ramadhan Sengati na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Miamala Benki ya NMB, Michael Mungure wakishiriki tukio hilo leo Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Meneja wa Idara ya Maboresho ya Ukusanyaji na Ulipaji Kodi TRA, Ramadhan Sengati (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa hafla ya kuingia makubaliano na Mamlaka ya Mapato (TRA) na NMB kukusanya kodi za TRA kupitia mfumo wa kibenki wa NMB. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Miamala Benki ya NMB, Michael Mungure pamoja na Meneja Huduma za Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili (kushoto) wakishiriki tukio hilo leo Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.