Gari ya Mzunguko a.k.a Daladala limegongana uso kwa uso na Bajaji eneo la Mwaji Uyole Jijini Mbeya kutokana na kile ambacho mashuhuda wameelezea kuwa ni ubabe wa madereva wote kuzidiwa kutokana na mwanga mkali wa taa waliowashiana na kupelekea kupoteza muelekeo kisha kugongana usiku huu...

Bajaji iliyogongana na Gari ya Mzunguko al maarufu kwa Jina la Daladala linalotoka Stendi kuu ya Soko Matola kuelekea Uyole Igawilo ikiwa nyang'anyang'a baada ya kugongana uso kwa uso eneo la Mwaji Uyole Jijini Mbeya usiku huu.
