Friday, July 15, 2016

NEWS ALERT: WAZIRI NAPE AANZA KULA SAHANI MOJA NA WAHARAMIA WA KAZI ZA WASANII NCHINI




NEWS ALERT: WAZIRI NAPE AANZA KULA SAHANI MOJA NA WAHARAMIA WA KAZI ZA WASANII NCHINI
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akiwa katika Operesheni ya kuwasaka waharamia wanaodurufu kazi za wasanii mbalimbali nchini, hali inayopelekea wasanii hao kazi zao kuzorota. Waziri Nape leo ameianza Operesheni hiyo kwa kutembelea Maduka mbalimbali yaliopo eneo la Kariakoo, Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akisimamia zoezi la ukusanyaji wa kazi zilizodurufiwa na wafanyabiashara hao katika moja ya Maduka yaliopo eneo la Kariakoo, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akimsikiliza mmoja wa watuhumiwa wa kudurufu kazi za wasanii, aliekuwa na mitambo ya kufanyia kazi hizo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa Kariakoo wakati wa Operesheni ya kuwasaka wanaodurufu kazi za wasanii mbalimbali nchini.


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

SERIKALI imesema inapoteza kodi nyingi kwa waagizaji wa filamu kutoka nje ya nchi na zikiingia hazilipi kodi na kusababisha kazi za wasanii wa ndani kukosa soko.

Kutokana na kupoteza kodi hizo serikali imeanza operesheni kwa filamu za nje kuwekewa stika za TRA na mtu ambaye atakutwa na filamu isiyo na stika atakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika Operesheni ya kukagua maghala yanayodaiwa kuwa na filamu za nje, Waziri wa Habari , Utamaduni , Michezo na Sanaa, Nape Nnauye amesema kuwa kazi wasanii wa ndani hazina soko kutokana na kuzagaa kwa filamu za nje ambazo hazilipi kodi.

Amesema kuwa wasanii wa ndani wamekuwa na majina lakini hawana kitu mfukoni kutokana na wahuni wachache wanaoingiza filam bila kulipa kodi na kuuza kwa bei ya chini. Katika operesheni hiyo wamefunga duka moja linalodaiwa kazi kubwa ni kutengeneza filam za nchi katika kunakrisha na watafungulia pale tu watapopata uhakika duka hilo.

Nape amesema barabara zinatakiwa kujengwa, Hospitali zinatakiwa kuwa na dawa hivyo bila kuwepo nguvu ya watu kulipa kodi bajeti haiwezi kufikiwa. Aidha amesema kuwa kutokana kuingizwa kwa kazi hizo bila utaratibu watato wanalishwa sumu mbaya ambayo ni tofauti na maadili ya kitanzania.

Waziri huyo amesema kuwa kazi za nje lazima zifuate utaratibu kwa kukaguliwa na kuwekewa stika za TRA .



BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI