MBUNGE MWAMOTO AIBUA UFISADI WA MWENDOKASI WA PESA ZA MADAWATI YA MFUKO WA JIMBO |
Madawati yaliyotengenezwa kwa pesa za mfuko wa jimbo la Kilolo ambayo mbunge Mwamoto ameyakataa kutokana na kukosa ubora ukilinganisha na thamani ya pesa iliyotumika |
|
Mbunge Mwamoto katikati akikimbia kwenda kukagua madawati katika kijiji cha Nyanzwa leo |
|
Kazi ya kuwatumikia wananchi ni ya mwendokasi zaidi |
|
Mbunge wa Kilolo Bw Venance Mwamoto akikagua madawati yaliyotengenezwa kwa pesa za mfuko wa jimbo |
|
Mwamoto akitazama madawati yaliyotengenezwa chini ya kiwango |
|
Haya ndio madawati yaliyotengenezwa kwa pesa za mfuko wa jimbo la Kilolo ila yapo chini ya kiwango |
|
Madawati ya kisasa yaliyotengenezwa kwa michango ya wanakijiji ambayo yametengenezwa kwa gharama ndogo kwa ubora mkubwa |
|
Wananchi wa Nyanzwa wakiwa katika mkutano wa kimaendeleo na mbunge wao |
|
Mbunge Venance Mwamoto akipinga madawati kutengenezwa chini ya kiwango |
madawati yaliyotengenezwa na kijiji kwa Tsh 20,000 madawati yaliyochini ya kiwango yaliyotengenezwa na ofisi ya Mbunge ambayo yamechakachuliwa kila moja limechongwa kwa Tsh 50,000
Na Matukiodaimablog
HOFU ya kutafunwa kwa fedha milioni 30 zilizotolewa na mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto kuchonga madawati imetanda baada ya mbunge huyo kuibua ufisadi wa mwendokasi na kulazimika kuyakataa madawati 40 yaliyotengenezwa kwa fedha za mfuko wa jimbo yaliyopelekwa kijiji cha Nyanzwa na Halmashauri kuwa hayana ubora.
Mbunge Mwamoto amesema kuwa hajapendezwa na kiwango cha utengenezaji wa madawati hayo ambayo ni mabovu na upo uwezekano wa kuharibika zaidi ndani ya siku mbili baada ya wanafunzi kuanza kutumia. Akizungumza leo na wananchi wa kijiji cha Nyazwa baada ya kukagua madawati hayo yaliyotengenezwa kwa pesa za mfuko wa jimbo ,kuwa hajapendezwa na ubora wa madawati hayo na hatakuwa tayari kupokea madawati hayo.
Kwani alisema ofisi yake imetoa fedha za kutengeneza madawati kwa ajili ya kusaidia kupunguza kero za madawati katika shule za wilaya hiyo ya Kilolo lengo ni kuona wanafunzi hawapati tena kero ya madawati.
Mbunge huyo alisema kuwa ametoa jumla ya Tsh milioni 30 kutoka mfuko wa jimbo kwa ajili ya madawati 600 ili kiwango cha madawati hayo 40 ambayo yamepelekwa kijiji cha Nyanzwa hajafurahishwa nacho.
Hivyo ameutaka uongozi wa serikali ya kijjji hicho kutokubali kupokea madawati hayo ambayo yapo chini ya kiwango kwani hayupo tayari kuona watu wanachakachua fedha hizo.
Mwamoto alisema haiwezekani madawati ya kijiji yaliyotengenezwa kwa Tsh 20,000 yakawa bora zaidi kuliko madawati ya mfuko wa jimbo ambayo yametengenezwa kwa gharama kubwa ya Tsh 50,000 kwa kila dawati.