Thursday, June 30, 2016

WATOTO WA KIPALESTINA WASHIKILIWA MATEKA ISRAEL


WATOTO WA KIPALESTINA WASHIKILIWA MATEKA ISRAEL
Sheria za kimataifa hususani kipengele cha 16 cha mkataba wa kimataifa wa kulindwa kwa haki za Mtoto duniani zinaonekana kuvunjwa nchini Israel ambako nchi hiyo inawashikilia mateka Watoto wa Kipalestina wanaokadiriwa kufikia 438 katika magereza yao.

Habari kutoka katika kituo cha utafiti wa mateka wa Kipalestina kinadai kuwahivi karibuni mtoto wa kipalestina Shadi Faraj mwenye umri wa miaka 12 alifikishwa kwenye mahakama moja nchini Israel kwa mara ya tatu na kesi yake kuahirishwa bila kujulikana hasa kosa la mtoto huyo ni lipi.

Kwa mujibu wa mkuu wa kitengo cha habari wa kituo hicho Riyadh Ashqar,amesema katika ripoti yake aliyoituma kwenda kwa manasaba wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupambana na mateso (QUDS) kwamba utwala wa kizayuni wa Israel unatumia mbinu 80 za mateso ya kimwili na kiroho dhidi ya mateka wa Kipalestina.

Ripoti ya hivi karibuni ya mfuko wa Watoto wa U moja wa Mataifa (UNICEF) inaonesha kuwa utawala wa kizayuni wa Israel ndiyo utawala pekee duniani unaowapandisha kizimbani kwa makusudi na kwa lengo maalumu, watoto wadogo tena kwenye mahakama za kijeshi.

Siku hii ya kimataifa ya QUDS huadhimishwa kila mwaka siku ya Ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hii ina maana kesho ndiyo siku yenyewe.