Friday, April 08, 2016

NWANKO KANU ATEMBELEA WAGONJWA WA MOYO MUHIMBILI



NWANKO KANU ATEMBELEA WAGONJWA WA MOYO MUHIMBILI
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles Nwankwo Kanu leo ametembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hopsitali ya Taifa Muhimbili (NH) kwa lengo la kuwajulia hali wagonjwa wa moyo ambao wamelazwa katikaTaasisi hiyo, pia kubadilishana uzoefu kuhusu huduma za matibabu zinazotolewa na wataalamu wa tasisi hiyo.
Akizungumza  baada ya kuwasili katika Taasisi hiyo Kanu ameelezea kuguswa na tatizo la ugonjwa wa moyo hasa kwa watoto wadogo ambao amewatembelea na kuwapa pole.
Katika mazungumzo yake pamoja na mambo mengine Kanu ameonyesha nia ya kushirikiana na watalaamu wa Taasisi ya Moyo ili kuwasaidia matibabu watoto wenye matatizo ya Moyo ambao wazazi wao hawana uwezo na kwamba watazungumzia suala hilo.
Pia, ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa Watanzania hasa wanamichezo kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara kwani ukijua tatizo mapema ni rahisi kupata matibabu na kupona.
Kwaupande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Godwin Godfrey amesema tangu Julai mwakaja na mpaka sasa taaissi hiyo kwa kushirikiana na wataalam kutoka nje ya nchi wamewafanyia upasuaji watoto zaidi ya 200.
Nwankwo Kanu alifanyiwa upasuaji wa moyo mwaka 1996 na ndipo aliamua kufungua taasisi yake ya moyo inayoitwa The Kanu Heart Foundation.
Kanu amechezea timu ya Taifa ya Nigeria yaSuper Eagles, Arsenal, Inter Milan, West Bromwich Albion, Portsmouth na AFC Ajax. Amenyakua tuzo nyingi kutokana na umairi wake soka.

 Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Arsenal, Inter Milan, West Bromwich Albion, Portsmouth na AFC Ajax,Nwankwo Kanu akilakiwa na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo, Dk Peter Kisenge, katika taasisi hiyo akimkaribishaNwankwo Kanu leo. katika Jengo la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete lililopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako amewatembelea wagonjwa wa moyo leo.

 Fatuma Shaban akipokea zawadi kutoka kwa Nwankwo Kanu kwa niaba ya mtoto wake, Ramadhan Shaban ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo kwenye taasisi hiyo.
 Mgonjwa Mariam Omary akifurahia jambo baada ya mchezaji huyo kumjulia hali leo kwenye taasisi hiyo.
 Mchezaji huyo akiwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) leo.
Kanu akipata maelezo kuhusu Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hopsitali ya Taifa Muhimbili 
Mchezaji huyo akieleza historia fupi baada ya kubainika kuwa na tatizo la moyo miaka ya tisini na kutokana na tatizo hilo aliamua kuanzisha mfuko wa kusaidia watu wenye matatizo ya moyo. Mfuko huo unajulikakanaKanu Heart Foundation.
Picha zote na John Stephen, Ofisa Uhusiano 
wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)