Friday, April 22, 2016

MKURUGENZI Mkuu wa Zamani wa Mamlaka ya Bandari Tanzania na naibu wake wana kesi ya kujibu - Mahakama ya Kisutu



MKURUGENZI Mkuu wa Zamani wa Mamlaka ya Bandari Tanzania na naibu wake wana kesi ya kujibu - Mahakama ya Kisutu
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) Ephraimu Mgawe (Kulia) na Makamu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hamadi Koshuma.
-------------------------------------------------------------
MKURUGENZI Mkuu wa Zamani wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe na Naibu Mkurugenzi Mkuu wake,  Hamadi Koshuma wana kesi inayowakabili ya kujibu dhidi ya mashtaka ya kesi ya matumizi mabaya ya madaraka wameonekana wana kesi ya kujibu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hatua hiyo ilifikiwa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Mhe. Cyprian Mkeha, anayesikiliza kesi hiyo baada ya kusikiliza ushahidi wa Jamhuri wa mashahidi watano. 
Hakimu huyo lisema baada ya kusikiliza ushahidi wa Jamhuri, kuita mashahidi watano dhidi ya kesi hiyo, mahakama yake imeona wana kesi ya kujibu. 
Hakimu alisema washtakiwa wanatakiwa kupanda kizimbani kujitetea ili kuondoa maswali katika ushahidi ulioacha mashaka dhidi yao. 
Alisema washtakiwa wataanza kujitetea Mei 16, mwaka huu na dhamana zao zinaendelea.
Katika kesi ya msingi, Desemba 5, mwaka 2011, washtakiwa wakiwa watumishi wa umma, katika utendaji wao wakazi kwa makusudi walitumia madaraka yao vibaya kwa kusaini mkataba wa kibiashara bila kuitisha zabuni.
Ilidaiwa kuwa mkataba huo ulikuwa kati ya TPA na Kampuni ya ujenzi ya Communication and Construction ya China (CCCC), ambao ulikuwa unahusu ujenzi wa gati namba 13 na 14 katika bandari ya Dar es Salaam, bila kuitisha zabuni.
Ilidaiwa kuwa, kitendo hicho kiliipa faida Kampuni  hiyo ya China.