Mkurugenzi wa ASpro Capital, Isaya Shoki akizungumza na waandishi habari juu ya mkutano wa wajasiriamali na Wafanyabishara wakati utaofanyika Aprili 29 katika Ukumbu Ubungo Plaza leo,jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakimzikiliza Mkurugenzi wa ASPRO Capital, Isaya Shoki leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAJASIRIAMALI wanashindwa kufikia malengo kutokana na kukosa maarifa ya uendeshaji biashara zao hivyo wanahitaji wataalam wa kuwasaidia kwenye biashara zao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuruegenzi wa Aspro Capital Group, Isaya Shoki amesema kuwa wajasiriamali kutokana na kukosa maalifa na wataalam na mitaji ya uendeshaji wa biashara Aspro Capital Group imeamua kufanya mkutano wa wajasirimali wadogo na wafanyabiashara wa kati katika kutoa elimu juu jinsi ya kuwawezesha na hata kutatua changamoto zao za mitaji,na masoko utakaofanyika Aprili 29 katika ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza.
Shoki amesema kuwa Aspro Capital itaweka mawakala katika kila nchi ambapo wafanyabiashara wanaweza kupata masoko ya biashara zao na kuweza kufikia malengo yao.
Amesema wajasirimali baadhi yao wamekuwa hawana vigezo vya kupata dhamana kutoka taasisi za fedha kutokana na biashara zao kukosa michanganuo ya kuweza kupata dhamana hiyo.
Shoki amesema Aspo Capital imeanzisha uwekezaji wa hisa zisizosajiliwa katika kampuni mbalimbali ambapo kwa wajasirimali ni moja ya njia ya kuweza kufikia malengo.
Amesema wajasiriamali wakiweza kupata mifumo ya uendeshaji biashara wanaweza kulipa kodi kuliko kutokana kukosa mifumo hiyo.
Shoki amesema kuwa wataalam wanampango wa miaka 10 katika kuwekeza katika viwanda vya korosho,matunda ,Ngozi pamoja na Pamba ili nchi iweze kufikia uchumi wa kati.