Lundega akifafanua                jambo kwa umakini mbele ya Wanahabari (hawapo pichani).
        Lundenga amesema kuwa                katika uzinduzi wa msimu huo mpya,utawakutanisha wadau                mbalimbali wa tasnia ya Urembo wakiwemo Wabunifu wa                Mavazi,Mawakala wanaoandaa mashindano ya Miss Tanzania                katika ngazi mbalimbali hapa nchini.kama vile haitoshi                Lundenga alibainisha kuwa pia Wakurugenzi wa makampuni                mbalimbali ambao miongoni mwao wanatarajia kuwa Wadhamini                wa shindano hilo kwa mwaka huu.
        Katika kunogesha                uzinduzi huo utakaokuwa wa aina yake,Lundemga amesema kuwa                burudani kadhaa zitakuwepo akiwemo msanii wa kizazi kipya                Linah Sanga pamoja na msanii wa ngoma za asili Wanne Star.
        Lundenga alisema kuwa                mara baada ya uzinduzi huo kufanyika jijini Dar,utahamia                mkoa wa Arusha ambako pia kutakuwa na aina nyingine ya                uzinduzi," Uzinduzi huo ukikamilika itafuata ratiba ya                semina ya mawakala na kuanza kwa mashindano ya urembo                katika ngazi za vituo,Wilaya,Mikoa na Kanda",alisema                Lundenga.
        Amesema kuwa mpaka sasa                Wadhamini kadhaa wamejitokeza na kuonesha nia ya kutaka                kudhamini shindano hilo katika ngazi ya Taifa.Lundenga                ameyataja makampuni ambayo yamedhamini uzinduzi huo wa                shindano la urembo la Miss Tanzania 2016 kuwa ni Ramada                Resort Dar,Naf Beach hotel Mtwara,Kitwe General Trader,CXC                Africa,MMI Tanzania,Mwandago Investment Ltd,Break Point                pamoja na GSM Media. 
         
