Meneja Rasilimali Watu                wa kampuni ya saruji ya Lafarge ya jijini Mbeya Bryson                Tarimo akizungumza mara baada ya kukabidhi mifuko 1,000 ya                saruji kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya shule ya                Sekondari Iyunga ambayo hivi karibuni yaliteketea kwa                moto,Kampuni ya Lafarge imetoa mifuko ya saruji yenye                thamani ya shilingi milioni 14. 
                Mkuu wa shule ya                sekondari ya Iyunga Edward Mwantimo akitoa neno la                shukrani mara baada ya kukabidhiwa mifuko 1,000 ya saruji                kutoka kampuni ya Lafarge ya jijini Mbeya kwa ajili ya                ujenzi wa mabweni ya shule ya Sekondari Iyunga ambayo hivi                karibuni yaliteketea kwa moto ambapo pia alielezea madhara                yaliyotokana na moto uliosababisha kuungua kwa mabweni ya                wanafunzi wa shule hiyo. 
                Viongozi wa kampuni ya                saruji ya Lafarge wakiwa pamoja na watendaji wa                Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakati wa kukabidhi mifuko                1,000 ya saruji kwa ajili ya mabweni yaliyoteketea ya                shule ya Sekondari Iyunga. 
                Kaimu Mkurugenzi wa                Halmashauri ya Jiji la Mbeya Dkt. Samwel Lazaro(kushoto)                akipokea mifuko 1000 ya saruji kutoka kwa Meneja Uajiri                watu wa kampuni ya saruji ya Lafarge Bryson Tarimo kwa                ajili ujenzi wa mabweni ya shule ya Iyunga yaliyoteketea                kwa moto hivi karibuni.
         Kampuni ya Saruji ya                Lafarge Tanzania (Mbeya Cement Company) imetoa msaada wa                zaidi ya mifuko 1,000 ya saruji na vifaa vingine vya                ujenzi kwa shule ya Sekondari ya Iyunga mkoani Mbeya                kufuatia mabweni ya shule hiyo kuungua moto hivi karibuni.
        Mashine ya kampuni                hiyo pia itatumika kufyatua zaidi ya matofali 40, 000                yanayohitajika kukamilisha ujenzi huo na kufanya jumla ya                msaada huo kuwa na thamani ya shilingi 14 milioni.                Akizungumza kwenye makabidhiano ya msaada huo, Meneja                Rasilimali Watu wa Lafarge Tanzania, Bryson Tarimo alisema                "tulipata habari za kushtusha kuhusiana na tukio la moto                ambao uliteketeza miundombinu ya shule pamoja na mali za                wanafunzi. 
        Tunatambua kwamba huu                umekuwa ni wakati mgumu kwa uongozi wa shule pamoja na                wanafunzi." Aliongeza kusema kwamba Lafarge inaamini                kwamba elimu ni muhimu kwa maendeleo ya mustakabali wa                Tanzania na pia kwamba elimu itasaidia kufungua mianya ya                fursa mbalimbali kwa Watanzania. Tarimo alieleza kwamba                Lafarge ina jukumu la kujenga mabweni hayo ili                kuwarudishia wanafunzi wa Sekondari ya Iyunga mazingira                mazuri ya kujisomea. "Hii ni sehemu ya jukumu letu                kuifikia jamii na kuisaidia jamii pamoja na taasisi                mbalimbali zilizopo mahali tunapofanyia kazi."
         Aliongeza: "Uhusiano                wetu na shule hii ni mkubwa sana kwa sababu tunaelewa                imewafundisha baadhi ya watu ambao hivi sasa wanaendesha                kiwanda chetu na kutufanya tuendelee kuwa na mafanikio.                Tunataka kuona wanafunzi wakirejea madarasani na walimu                wakiendelea kutimiza majukumu yao kama kawaida kwani azma                yetu ni kuona shule hii inapata mafanikio na kuwapa                wanafunzi fursa ya kutimiza ndoto zao na kuwa na                mustakabali mzuri. 
        Mtazamo wetu ni kuona                Tanzania ikiwa nchi inayotoa fursa ya elimu kwa kila mtoto                ili watoto hawa wote kila mmoj aweze siku moja kuchangia                maendeleo ya nchi hii." Tarimo alisema kwamba Lafarge                inajali maendeleo ya jamii na ina fahari kuweza kutoa                msaada huu kwa shule ya Sekondari ya Iyunga kufuatia moto                ulioteketeza mabweni ya shule hiyo. 
        Tunaamini msaada huu                utarejesha hali ya kawaida katika shule hii na sisi kama                sehemu ya jamii hii tunapenda kuona wanafunzi hawa                wakiishi katika mazingira salama." Tarimo aliyaomba                makampuni mengine na taasisi mbalimbali, watu binafsi na                jamii kwa ujumla kuisaidia ujenzi wa shule hiyo.
         
