Thursday, March 17, 2016

JAJI JALLOW AMUAGA WAZIRI MWAKYEMBE


JAJI JALLOW AMUAGA WAZIRI MWAKYEMBE
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya mauaji ya halaiki ya Rwanda (ICTR) Jaji Hassan B. Jallow anayemaliza muda wake. Jaji Jallow alifika ofisini kwa Mhe. Mwakyembe leo (17/3/2016) kwa ajili ya kumuaga rasmi.
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya halaiki ya Rwanda (ICTR) Jaji Hassan B. Jallow (kulia) anayemaliza muda wake akifurahia jambo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe alipomtembelea leo (17/3/2016)ofisini kwake kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa kazi kwenye Mahakama hiyo.