Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Bakari akiwashukuru wadau hao wakiwamo mabalozi kutoka Israel na Ujerumani na wadau wengine kwa misaada mbalimbali wanayoitoa katika taasisi hiyo. Leo Profesa Bakari amewataka madaktari na wauguzi wa taasisi hiyo kutumia vizuri nafasi mbalimbali za mafunzo kutoka kwa wadau hao wa afya.
Naibu Balozi wa Israel, Nadar Peldman akizungumza na madaktari, wauguzi na wadau mbalimbali wa sekta ya afya baada ya kuwatembelea watoto waliofanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Muhimbili. Jana watoto wanne walifanyiwa upasuaji na leo watoto sita wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji kwenye taasisi hiyo.
Kulia ni Naibu Balozi wa Ujerumani, John Reyels akizungumza leo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kushoto) baada ya naibu balozi huyo kuwatembelea watoto waliofanyiwa upasuaji wa moyo jana. Katikati ni Rais wa Rotary Club jijini Dar es Salaam, Zainul Dossa.
Baadhi ya madaktari na wauguzi wa taasisi hiyo wakimsikiliza Naibu balozi wa Israeli na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Bakari Leo pamoja na wageni wengine.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Save Child's Heart (SACH), Simon Fisher kutoka nchini Israel akizungumza leo baada ya kufuatilia shughuli ya upasuaji wa watoto ambayo imeanza jana katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Muhimbili. Kushoto ni Rais wa Rotary Club nchini Tanzania, Sharmila Bhatt.
Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi akishukuru mabalozi, wawakilishi wa BAPS Charities, madaktari kutoka Israel na wadau wengine kwa misaada mbalimbali ambao wamekuwa wakisadia kufanikisha shughuli za upasuaji wa moyo kwenye taasisi hiyo.