Katika kudumisha urafiki mwema kati ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (JKCI) na Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko jijini Tel Aviv, Israel, Kaimu Mkurugenzi wa JKCI Profesa Mohamed Janabi amefanya ziara kutembelea hospitali hiyo na kuonana na madaktari bingwa wa moyo pamoja na watoto wa Kitanzania kadhaa waliopewa rufaa kwenda kupata matibabu hapo.
Profesa Janabi ameiambia Globu ya Jamii kwa njia ya simu kutoka Tel Aviv kuwa Serikali ya Israel kupitia mpango wake wa Save a Child's Heart (Okoa moyo wa mtoto) ni moja ya washirika wakubwa wa JKCA katika kubadilishana utaalamu na vifaa.
"Washirika wetu wengine ni Open Heart international ya Australia, Mending Kids Heart ya California, Madaktari Africa ya South Carolina, Almutada ya Saudi Arabia, Sharjah International ya UAE na Madras Medical mission and BLK ya India.
"Hawa wote kwa muda mbalimbali huw wanakuja JKCI na mpaka sasa katika mwaka huu wa 2016 wamekuja BLK, Madaktari Africa na lsrael" alisema, na kuongezea kuwa "Kwenye hospital ya moyo ya Wolfson tunayoshirikiana nayo JKCI. Nimeona watoto wetu 11 tuliowaleta huku wakiwa na complicated cases. Tisa wamekwisha fanyiwa upasuaji bado wawili na wote wanatokea Zanzibar.
Profesa Janabi ameongozana na manesi watatu na daktari mmoja.
Kaimu Mkurugenzi wa JKCI Profesa Mohamed Janabi baadhi ya wenyeji wake katika Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko jijini Tel Aviv, Israel, wakati wa ziara yake
Kaimu Mkurugenzi wa JKCI Profesa Mohamed Janabi akiwa na madaktari bingwa wa moyo katika Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko jijini Tel Aviv, Israel, wakati wa ziara yake
Kaimu Mkurugenzi wa JKCI Profesa Mohamed Janabi akiongea na Mkuu wa Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko jijini Tel Aviv, Israel, wakati wa ziara yake
Kaimu Mkurugenzi wa JKCI Profesa Mohamed Janabi akiwa ametoka kusaidia upasuaji na madaktari bingwa wa moyo katika Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko jijini Tel Aviv, Israel, wakati wa ziara yake
Kaimu Mkurugenzi wa JKCI Profesa Mohamed Janabi akiwa na baadhi ya wagonjwa na walezi wao waliofanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko jijini Tel Aviv, Israel, wakati wa ziara yake. Bango aliloshika linaonesha majina ya wagonjwa kutoka Tanzania waliofanyiwa upasuaji