Hatua nyingine kubwa imefikiwa leo hii katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda kupitia Kaskazini mwa Tanzania hadi bandari ya Tanga.
Katika kikao kazi kilichofanyika jijini Arusha, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, Waziri wa Maendeleo ya Nishati na Madini-Uganda, Mhandisi Irene Muloni, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio na Meneja Mkuu wa Total E&P Uganda, Ndugu Adewale Fayemi wametia saini mpango wa pamoja wa utekelezaji wa mradi huo (Project Implementation Plan).
Hatua hii imekuja ikiwa ni wiki mbili tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kutoa tamko la pamoja la utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda kupitia mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma hadi bandari ya Tanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (wa kwanza kushoto), Waziri wa Nishati na Madini-Tanzania, Prof. Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kushoto), Waziri wa Maendeleo ya Nishati na Madini-Uganda, Mhandisi Irene Muloni ( wa tatu kutoka kushoto), Meneja Mkuu wa Total E&P Uganda, Adewale Fayemi (wa nne kutoka kushoto) wakitia saini mpango wa pamoja wa utekelezaji wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga. Kulia kabisa ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Nishati na Madini-Uganda, Dkt. Kabagambe Kaliisa
Waziri wa Nishati na Madini-Tanzania, Prof. Sospeter Muhongo na Waziri wa Maendeleo ya Nishati na Madini-Uganda, Mhandisi Irene Muloni wakibadilishana nyaraka baada ya kutia saini kwa pamoja
Waziri wa Nishati na Madini-Tanzania, Prof. Sospeter Muhongo na Waziri wa Maendeleo ya Nishati na Madini-Uganda, Mhandisi Irene Muloni wakionesha nyaraka zenye mpango kazi wa pamoja kati ya Tanzania, Uganda na Kampuni ya Total na TPDC juu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga.