Hakuna kazi isiyokuwa na ugumu,watunzi na waimbaji wa muziki nao wanakumbana na ugumu katika kazi zao,mmoja wao kati ya wanamuziki wanaopata misuko suko kazini ni mwanamuziki nguli Ebrahim Makunja almaarufu Kamanda Ras Makunja mkuu wa kikosi cha Ngoma Africa band aka FFU wenye maskani yao kule Ujerumani.
Mwanamuziki mtanzania Kamanda Ras Makunja, mtunzi,mshairi na mwimbaji aliyepindia akili kazi yake, ametunga na kuimba nyimbo nyingi zenye utamu na uchungu,lakini katika nyimbo zote wimbo wa "Baba wa Kambo" ni wimbo uliompa wakati mgumu sana,mara tatu kutafutwa na bakora na wazee walioguswa na wimbo huo, akiwamo mtu mzima Malumba Kassongo alishawahi mara mbili kuvamia kambi ya bendi hiyo kwa bakora na kudai kuwa kamanda Ras Makunja lazima atiwe adabu kwani mdomo wake si mzuri, mzee huyo amedai mtunzi wa nyimbo hiyo "Baba wa Kambo" amekuwa akiyachunguza maisha ya mzee huyo.
pamoja na makubaliano mbele ya wapatanishi kuwa nyimbo hiyo isiende hewani lakini bendi hiyo imekiuka makubaliano na kurusha hewani tena song hilo "Baba wa Kambo" jiburudishe na song hilo chini.