Mshambuliaji wa Azam FC, Allan Wanga akiwatoka mabeki wa Stand United wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam leo, Azam imeshinda 1-0. (Picha na Francis Dande)
Beki wa Stand United, Assouman N'guessan (kulia) akichuana na mshambuliaji wa Azam FC, Allan Wanga.
Kipa wa Stand United, Frank Muwange akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche akitafuta mbinu ya kumtoka beki wa Stand United, Assouman N'guessan wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
Mashabiki Stand United wakifutilia pambano hilo.

Golikipa wa Azam FC, Aishi Manula akidaka mpira langoni pake.