Saturday, December 12, 2015

WAZIRI UMMY MWALIMU NA NAIBU WAKE DK. KIGWANGALA WARIPOTI WIZARANI LEO


WAZIRI UMMY MWALIMU NA NAIBU WAKE DK. KIGWANGALA WARIPOTI WIZARANI LEO
IMG_8317
Gari la Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu likiwasili Makao Makuu ya wizara hiyo na kupokelewa kwa saluti mara tu baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli katika sherehe zilizofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_8321
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando mara tu baada ya kumalizika kwa tukio la kuapishwa.
IMG_8324
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongozana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando (kulia) kuelekea ofisini kwake.
IMG_8325
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo.
IMG_8329
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wageni ofisini kwake huku Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando akishuhudia tukio hilo.
IMG_8346
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwasili katika wizara ya hiyo moja kwa moja akitokea Ikulu baada ya kula kiapo.
IMG_8347
Pichani juu na chini ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo.
IMG_8350
IMG_8354
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akimkaribisha Naibu wake Dkt. Hamis Kigwangala ofisini kwake.
IMG_8356
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala ofisini kwa Mh. Ummy Mwalimu.
IMG_8359
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mh. Ummy Mwalimu.
IMG_8374
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando akitoa taarifa ya maendeleo ya Wizara kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu na Naibu wake Dkt. Hamis Kigwangala. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Gideon Malabeja.