Rais Dkt. John                  Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Charles Kitwanga                  (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ikulu jijini Dar                  es salaam leo. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu                  Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
         Makamu wa Rais                  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu                  Hassan (kushoto) akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya                  Nchi, Charles Kitwanga, mara baada ya kuapishwa Ikulu                  jijini Dar es Salaam leo.
         Waziri Mkuu Mhe                  Majaliwa Kassim Majaliwa (kushoto) akimpongeza Waziri wa                  Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, mara baada ya                  kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
         Waziri wa Mambo                  ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akiteta                  jambo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil                  (kulia) na Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo mara baada ya                  kumpongeza Waziri huyo mpya, nje ya Ukumbi wa Mikutano                  Ikulu, jijini Dar es Salaam.
         Naibu Katibu                  Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo                  (kulia) akimkaribisha wizarani Waziri mpya wa Mambo ya                  Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga mara baada ya kuapishwa                  Ikulu, jijini Dar es Salaam leo.
         Katibu Mkuu wa                  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil                  (kushoto) akimkaribisha Waziri mpya wa Mambo ya Ndani ya                  Nchi, Charles Kitwanga, ndani ya ofisi ya waziri huyo                  iliyopo Mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam.
         Waziri wa Mambo                  ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akisaini kitabu cha                  wageni kilichopo ndani ya ofisi yake, mara baada ya                  Waziri huyo mpya kuingia ndani ya ofisi hiyo baada ya                  kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
         Katibu Mkuu wa                  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil                  (wapili kushoto) akimfafanulia Waziri mpya wa Wizara                  hiyo, Charles Kitwanga (kulia), shughuli mbalimbali                  zinazofanywa na wizara hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu                  Mkuu, John Mngodo. Tukio hilo lilifanyika katika Ukumbi                  wa Mikutano wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, mara                  baada ya Waziri huyo kuapishwa Ikulu leo. 
                Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles                  Kitwanga (kulia) akijadiliana na watendaji wa wizara                  hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya wizara hiyo, mara                  baada ya Waziri huyo kuapishwa Ikulu jijini Dar es                  Salaam leo. Wanne kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,                  Mbarak Abdulwakil, anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu, John                  Mngodo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP),                  John Minja, Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi (D/IGP),                  Abdurahman Kaniki na Kamishina wa Fedha na Utawala wa                  Idara ya Uhamiaji, Piniel Mgonja (hayupo pichani). 
        Picha zote na Felix Mwagara, Kitengo cha                  Mawasiliano-MOHA.
         
