Habari na picha na Ismail Ngayonga - MAELEZO
SERIKALI imewataka watumishi wa sekta ya afya nchini kutofanya kazi kwa mazoea na badala yake kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kufikia malengo yaliyowekwa. Hatua hiyo inaelezwa itasiaidia kurahisisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi kwa kutoa huduma bora na zinazofikiwa kwa wakati.
Akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema kila mtumishi wa umma anapaswa kutekeleza kwa bidii ilani ya Chama Tawala ya mwaka 2015.
"Sekta ya Afya imeingizwa kwenye mpango wa Tekeleza kwa Matokeo makubwa sasa, ili tuyakifia matokeo makubwa sasa pamoja na mambo mengine tunahitaji kubadilika sana katika utendaji wetu wa kazi" alisema Mwalimu.
Aidha Waziri huyo alisema alisema pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa katika sekta ya afya, Wizara hiyo hiyo hiyo haina budi kuakabiliana na chyangamoto mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo vifo vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua.
Kwa mujibu wa Waziri Mwalimu aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kutekeleza kwa vitendo maagizo yaliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hotuba yake ya kuzindua Bunge la 11, kwani hotuba yake ni dira ya maelekezo rasmi ya masuala muhimu yanayopaswa kutekelezwa na kusimamiwa katika kipindi cha miaka mitano.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando alisema katika kutekeleza mpango wa tekeleza kwa matokeo makubwa sasa, Serikali imeanisha maeneo 4 ya utekelezaji ili kuboresha huduma bora za afya kwa wanachi.
Dkt. Mmbando alianisha maeneo hayo kuwa ni pamoja mgawanyo wa watumishi wa kada ya afya, upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi, ubora wa huduma pamoja na kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.
"Katika kutekeleza haya, wiki ijayo tutazindua mpango mkakati wa miaka 5 wa sekta ya afya (2016-20), ambapo tutahakikisha kuwa yote yaliyoanishwa katika Ilani ya Chama Tawala tunaweza kuyafikia na kuyatekeleza" alisema Dkt. Mmbando
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando na wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamis Kigwangalla.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando na kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamis Kigwangalla.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam.
1. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mara baada ya kulifungua Baraza hilo leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamis Kigwangalla (wa tano kutoka kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando.