Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Vodacom imekidhi vigezo vya utoaji huduma kwa wateja huku makampuni matano yakipigwa adhabu ya sh.milioni 25 kutokana kulaghai wateja.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Nchini (TCRA), Dkt. Ally Simba amesema kuwa kampuni ambazo hazijaweza kuboresha huduma zao kuanzia leo ili kuweza wateja kupata huduma bila kuwepo kwa malalamiko.
Kampuni zilipigwa adhabu kutokana na kukiuka taratibu za kisheria za utoaji wa huduma za mawasiliano ni Tigo,Airtel,Halotel ,Zantel pamoja na Smart.
Simba amesema mitandao ya mawasiliano inaweka mazingira salama yatakyozuia utumaji wa ujumbe za kilaghai na matishio mengine ya kiusalama.
Amesema adhabu ya sh.milioni 25 kwa kampuni zilizokiuka sheria za utoaji wa huduma zinatakiwa kulipa kabla ya Januari 29.
Aidha TCRA imetaka kampuni ambazo zitashindwa kukidhi vigezo vilivyowekwa hawataacha kuwachukulia hatua za kisheria kwa kampuni husika.