Monday, March 07, 2016

TPDC na Jeshi la Polisi wafanya ziara ya kutembelea miundombinu- Mtwar hadi Dar



TPDC na Jeshi la Polisi wafanya ziara ya kutembelea miundombinu- Mtwar hadi Dar
Kwa kuzingatia umuhimu wa miundombinu kuchakata na kusafirisha gesi asilia hapa nchini, Serikali imedhamiria kuimarisha zaidi ulinzi wa miundombinu hii.

Haya yalibainishwa mwishoni mwa juma ambapo Mkuu wa Jeshi la polisi Tanzania, IGP Ernets Mangu alifanya ziara kutembelea miundombinu ya gesi asilia kutokea Mtwara mpaka Dar es Salaam. 

Katika ziara hiyo, IGP aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dr. James Mataragio, ambapo kwa pamoja walipata fursa ya kuona visima vinavyozalisha gesi vilivyopo Mnazi Bay na baadae kutembelea kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba na baadhi ya "Block Valve Statio-BVS" ambazo zina matoleo kwa ajili ya kuruhusu ugawaji wa gesi asilia maeneo ambayo yatahitaji hapo baadae.

IGP Magu aliipongeza TPDC kwa jitihada ilizofanya za ulinzi shirikishi na kusisitiza kwamba wananchi ndio walinzi wa kwanza wa miundombinu hii.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Ernest Mangu akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio pamoja na wataalamu kutoka Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Maurel and Prom inayoendeleza gesi asilia katika kitalu cha Mnazi Bay.
Meneja Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba, Mhandisi Kassim Mkombwa akitoa maelezo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Ernest Mangu na waliombatana nae wakati wa ziara ya kutembelea miundombinu ya gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Ernest Mangu akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu (hayuko pichani) wakati wa ziara ya kutembelea miundombinu ya gesi asilia kuanzia Mtwara hadi Dar es Salaam.