Thursday, December 24, 2015

MTU MMOJA ALA KICHAPO KWA TUHUMA ZA KUJIDAI AFISA WA TRA


MTU MMOJA ALA KICHAPO KWA TUHUMA ZA KUJIDAI AFISA WA TRA
Camera  imelinasa tukio la baadhi ya Raia wenye hasira waliokuwa wakilishambulia gari la mtu mmoja lenye namba za usajili T945 BYG,na pia kumpa kipigo mtu huyo aliyetuhumiwa kuwa ni tapeli .

Mtu huyo alijitambulisha kuwa ni Afisa wa TRA,lakini akatuhumiwa kuwa ni tapeli aliyetaka kufanya tukio la kiuhalifu kwenye moja ya Maduka yaonekayo mbele ya gari hilo,tukio hilo limetokea hivi punde maeneno ya Tabata Segerea. Mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika  mapema,amekamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi Tabata Segerea kwa hatua zaidi za kisheria