Marehemu Eng. John Said Kimbe
Jumuiya ya Watanzania Mozambique (JUWAMO) inasikitika kutangaza kifo cha Ndugu yao Mpendwa Eng. John Said Kimbe, kilichotokea ghafla usiku wa tarehe 10 Novemba, 2014 nyumbani kwake Maputo, Mozambique.
Wakati wa uhai wake, marehemu alikuwa Mwenyekiti wa JUWAMO, Tawi la CCM Maputo, Mozambique na Mfanyakazi; Mtaalamu wa Miundombinu ya Mawasiliano "Telecommunication/ICTs expert" kwenye Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC), kitengo cha "Southern Africa Telecommunications Association (SATA) tangu Juni 2001.
Jumuiya ya Watanzania Mozambique inawafahamisha Watanzania wote waishio Jiji la Maputo na vitongoji vyake kuwa mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa "Memorial Service" tarehe 13 Novemba, 2014 katika Kanisa la Roman Catholic "Paroquia Nossa Senhora das Victoria" Karibu na Soko la Janet – Maputo, saa 9. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda Tanzania kwa mazishi tarehe 14 Novemba, 2014.
JUWAMO inawaomba Watanzania wote kujitokeza kumuaga mpendwa wetu na kuwafariji wafiwa kama mila na desturi zetu zinavyotuelekeza.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Katibu wa JUWAMO Ndugu Annuar Aziz Simu No. +258824034391 au +258842337117 na Katibu wa CCM –Tawi la Maputo, Mozambique Ndugu Gesona Ngabo Simu No. +258821403433.
Imetolewa na JUWAMO
12/11/2014