Mkuu wa Kijiji cha Maeneo huru ya uwekezaji katika Mji wa Chengmai aliyevaa shati jeupe Bwana Yang Si Tao akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyepo kushoto yake wakati ujumbe wa Zanzibar ulipoangalia maeneo hayo ukiwa katika ziara ya siku 10 Jimboni Hainan. Kushoto ya Balozi ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo Haji,Balozi wa Tanzania Nchini China Bwana Abdullrahman Shimbo na Mkewe Mama Mary Antoni Tairo. Nyuma ya Bwana Yang Si Tao ni Waziri wa Habari Zanzibar Mh. Said Ali Mbarouk, Katibu Mkuu Fedha Nd. Khamis Mussa,Mye wa Manispaa ya Zanzibar Msitahiki Khatib Abdulrahman, Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala wa Mikoa na Idara Maalum Nd. Joseph Abdulla Meza, Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalis Salum Mohamed, Waziri wa Ardhi Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban, Mhudumu wa Balozi Seif Hassan Ali pamoja na Mkurugenzi Manispaa Nd. Abeid Juma Ali.
Balozi Seif na ujumbe wake wakifuatana na mwenyeji wao Mkuu wa Kijiji cha Uwekezaji wa Mji wa Chengmai Bwana Yang Si Tao wakielekea ukumbi wa mkutano kwa mazungumzo. Kulia ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Nd. Salum Nassor Khamis, Mkurugenzi Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo haji.
Ujumbe wa Zanzibar ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ule mwenjeji wa Hainan ukiongozwa na Gavana wa Jimbo hilo Bwana Jian Dingzhi ukiendelea na mazungumzo yao ya uhusiano hapo katika Hoteli ya Le Meriden Mjini Haikou.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi zawadi wa Kasha lililojaa vyakula vya viungo { spices } Gavana wa Jimbo la Hainan Bwana Jian Dingzhi mara baada ya kumaliza mkutano wao rasmi wa ushirikiano.
Gavana wa Jimbo la Kisiwa cha Hainan Bwana Jian Dingzhi akibadilishana mawazo na Mgeni wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.